Zaburi125swh_onmm
Usalama wa watu wa Mwenyezi Mungu
Wimbo wa kwenda juu.
1Wale wamtumainio Mwenyezi Mungu ni kama Mlima Sayuni,ambao hauwezi kutikisika, bali wadumu milele.2Kama milima inavyozunguka Yerusalemu,ndivyo Mwenyezi Mungu anavyowazunguka watu wakesasa na hata milele.3Fimbo ya waovu haitadumu juu ya nchiwaliyopewa wenye haki,ili wenye haki wasije wakatumiamikono yao kutenda ubaya.4Ee Mwenyezi Mungu, watendee mema walio wema,wale walio wanyofu wa moyo.5Bali wale wanaogeukia njia zilizopotoka,Mwenyezi Mungu atawafukuza pamoja na watenda maovu.Amani iwe juu ya Israeli.