Zaburi124swh_onmm

Shukrani kwa ukombozi wa Israeli

Wimbo wa kwenda juu. Wa Daudi.

1Kama Mwenyezi Mungu hangekuwa upande wetu;Israeli na aseme sasa:2kama Mwenyezi Mungu hangekuwa upande wetu,watu walipotushambulia,3hasira yao ilipowaka dhidi yetu,wangetumeza tukiwa hai,4mafuriko yangegharikisha,maji mengi yangetufunika,5maji yaendayo kasiyangetuchukua.
6Ahimidiwe Mwenyezi Mungu,ambaye hakuruhusu turaruliwe kwa meno yao.7Tumeponyoka kama ndegekutoka mtego wa mwindaji;mtego umevunjika,nasi tumeokoka.8Msaada wetu ni katika jina la Mwenyezi Mungu,Muumba wa mbingu na dunia.