Zaburi123swh_onmm

Kuomba rehema

Wimbo wa kwenda juu.

1Ninayainua macho yangu kwako,kwako wewe unayeketi mbinguni kwenye kiti chako cha enzi.2Kama vile macho ya watumwayatazamavyo mkono wa bwana wao,kama vile macho ya mjakaziyatazamavyo mkono wa bibi yake,ndivyo macho yetu yamtazamavyo Mwenyezi Mungu, Mungu wetu,hadi atakapotuhurumia.
3Uturehemu, Ee Mwenyezi Mungu, uturehemu,kwa maana tumevumilia dharau nyingi.4Tumevumilia dhihaka nyingi kutoka kwa wenye kiburi,dharau nyingi kutoka kwa wenye majivuno.