Zaburi12swh_onmm
Kuomba msaada
Kwa mwimbishaji. Mtindo wa sheminithi. Zaburi ya Daudi.
1Mwenyezi Mungu tusaidie, kwa kuwa wacha Mungu wametoweka;waaminifu wametoweka miongoni mwa wanadamu.2Kila mmoja humwambia jirani yake uongo;midomo yao ya hila huzungumza kwa udanganyifu.3Mwenyezi Mungu na akatilie mbali midomo yote ya hilana kila ulimi uliojaa majivuno,4ule unaosema, “Kwa ndimi zetu tutashinda;midomo ni mali yetu, bwana wetu ni nani?”5“Kwa sababu wanyonge wanaonewa,na wahitaji wanalia kwa uchungu,nitainuka sasa,” asema Mwenyezi Mungu.“Nitawalinda kutokana na walewenye nia mbaya juu yao.”6Maneno ya Mwenyezi Mungu ni safi,kama fedha iliyosafishwa katika tanuru,iliyosafishwa mara saba.7Ee Mwenyezi Mungu, utatuweka salamana kutulinda na kizazi hiki milele.8Watu waovu huenda wakiringa kila mahaliwakati yule aliye mbaya sanandiye anayeheshimiwa miongoni mwa watu.