Zaburi11swh_onmm

Kumtumaini Mwenyezi Mungu

Kwa mwimbishaji. Zaburi ya Daudi.

1Kwa Mwenyezi Mungu ninakimbilia.Unawezaje basi kuniambia:“Ruka kama ndege utorokee kwenye mlima wako.2Hebu tazama, waovu wanapinda nyuta zao;wanaweka mishale kwenye nyuzi zakeili wakiwa gizani, wawapigewalio wanyofu wa moyo.3Wakati misingi imeharibiwa,mwenye haki anaweza kufanya nini?”
4Mwenyezi Mungu yuko ndani ya Hekalu lake takatifu;Mwenyezi Mungu yuko kwenye kiti chake cha enzi mbinguni.Huwaangalia wana wa watu,macho yake yanawachunguza.5Mwenyezi Mungu huwachunguza wenye haki,lakini nafsi yake inachukia waovuna wale wanaopenda mapigano.6Atawanyeshea waovu makaa ya moto mkalina kiberiti kinachowaka;upepo wenye joto kali ndio fungu lao.
7Kwa kuwa Mwenyezi Mungu ni mwenye haki,yeye hupenda haki.Wanyofu watauona uso wake.