1Heri mtu yule ambaye haendikatika shauri la watu waovu,wala hasimami katika njia ya wenye dhambi,au kuketi katika baraza la wenye mizaha.2Bali huifurahia Torati ya Mwenyezi Mungu,naye huitafakari hiyo Torati usiku na mchana.3Mtu huyo ni kama mti uliopandwakando ya vijito vya maji,ambao huzaa matunda kwa majira yakena majani yake hayanyauki.Lolote afanyalo hufanikiwa.
Huzuni ya waovu
4Sivyo walivyo waovu!Wao ni kama makapiyanayopeperushwa na upepo.5Kwa hiyo waovu hawatastahimili hukumu,wala wenye dhambi katika kusanyiko la wenye haki.6Kwa maana Mwenyezi Mungu huziangalia njia za mwenye haki,bali njia za waovu zitaangamia.