Mithali25swh_onmm

1Hizi ni mithali zaidi za Sulemani, zilizonakiliwa na watumishi wa Hezekia mfalme wa Yuda:2Ni utukufu wa Mungu kuficha jambo,bali ni utukufu wa wafalme kuchunguza jambo.
3Kama mbingu zilivyo juu na nchi ilivyo chini,ndivyo ambavyo mioyo ya wafalme haichunguziki.
4Ondoa takataka kwenye madini ya fedha,na ndani yake kutatokea chombocha mfua fedha.5Ondoa waovu mbele ya mfalme,nacho kiti chake cha ufalmekitaimarishwa kupitia kwa haki.
6Usijikweze mwenyewe mbele ya mfalme,wala usidai nafasi miongoni mwa watu wakuu;7ni afadhali yeye akuambie, “Njoo huku juu,”kuliko yeye kukuaibisha mbele ya mkuu.Kile ulichokiona kwa macho yako8usiharakishe kukipeleka mahakamani,maana utafanya nini mwishonikama jirani yako atakuaibisha?
9Ukifanya shauri na jirani yako,usisaliti siri ya mtu mwingine,10ama yeye aisikiaye aweza kukuaibisha,na kamwe sifa yako mbaya haitaondoka.
11Neno lisemwalo kwa wakati ufaaoni kama matunda ya mtofaa ya dhahabuyaliyowekwa kwenye vijalizo vya fedha.
12Kama vile kipuli cha dhahabuau pambo la dhahabu safi,ndivyo lilivyo karipio la mtu mwenye hekimakwa sikio lisikilizalo.
13Kama vile ubaridi wa theluji wakati wa mavunondivyo alivyo mjumbe mwaminifu kwa wale wamtumao,huburudisha roho za bwana zake.
14Kama vile mawingu na upepo pasipo mvuandivyo alivyo mtu ajisifuye kwa zawadi ambazo hatoi.
15Kwa uvumilivu mtawala aweza kushawishiwa,nao ulimi laini unaweza kuvunja mfupa.
16Ukipata asali, kula kiasi tu cha kukutosha,ukila zaidi, utatapika.17Nenda nyumbani mwa jirani yako mara chache;ukizidisha, atakukinai na atakuchukia.
18Kama vile rungu au upanga au mshale mkalindivyo alivyo mtu atoaye ushuhuda wa uongo dhidi ya jirani yake.
19Kama vile jino bovu au mguu uliolemaa,ndivyo ilivyo kumtegemea mtu asiye mwaminifu wakati wa shida.
20Kama vile avuaye mavazi siku ya baridi,au kama siki iliyomwagwa juu ya magadi,ndivyo alivyo yeye amuimbiaye nyimbo mtu mwenye moyo mzito.
21Kama adui yako ana njaa, mpe chakula ale;kama ana kiu, mpe maji anywe.22Kwa kufanya hivyo, unaweka makaa ya motoyanayowaka kichwani pake,naye Mwenyezi Mungu atakupa thawabu.
23Kama vile upepo wa kaskazini uletavyo mvua,ndivyo ulimi usingiziao uletavyo uso wa hasira.
24Ni afadhali kuishi pembeni mwa paa la nyumba,kuliko kuishi nyumba moja na mke mgomvi.
25Kama vile maji baridi kwa nafsi iliyochokandivyo zilivyo habari njema kutoka nchi ya mbali.
26Kama vile chemchemi iliyotibuliwa matope aukisima kilichotiwa takandivyo alivyo mtu mwenye hakiakishiriki na waovu.
27Si vyema kula asali nyingi sana,wala si heshimakujitafutia heshima yako mwenyewe.
28Kama vile mji ambao kuta zake zimebomokandivyo alivyo mtuambaye hawezi kujitawala mwenyewe.