Mithali22swh_onmm
1Heri kuchagua jina jema kuliko utajiri mwingi;kuheshimiwa ni bora kuliko fedha au dhahabu.2Tajiri na maskini wanafanana kwa hili:Mwenyezi Mungu ni Muumba wao wote.3Mtu mwenye busara huona hatari na kujificha,bali mjinga huendelea mbele, naye hupata madhara.4Unyenyekevu na kumcha Mwenyezi Munguhuleta utajiri, heshima na uzima.5Katika mapito ya waovu kuna miiba na mitego,bali yeye ailindaye nafsi yake hukaa mbali nayo.6Mfundishe mtoto njia impasayo kuiendea,naye hataiacha hata akiwa mzee.7Matajiri huwatawala maskininaye akopaye ni mtumwa wa akopeshaye.8Yeye aupandaye uovu huvuna taabu,nayo fimbo ya ghadhabu yake itaangamizwa.9Mtu mkarimu yeye mwenyewe atabarikiwakwa kuwa hushiriki chakula chake na maskini.10Mfukuze mwenye dhihaka,na mvutano utatoweka;ugomvi na matukano vitakoma.11Yeye apendaye moyo safi na yeye ambaye maneno yake ni ya neema,mfalme atakuwa rafiki yake.12Macho ya Mwenyezi Mungu hulinda maarifa,bali huyapinga maneno ya asiye mwaminifu.13Mvivu husema, “Yuko simba nje!”au, “Nitauawa katika mitaa!”14Kinywa cha mwanamke kahaba ni shimo refu;yeye aliye chini ya ghadhabu ya Mwenyezi Munguatatumbukia ndani yake.15Upumbavu umefungwa ndani ya moyo wa mtoto,bali fimbo ya adhabu itaufukuzia mbali naye.16Yeye anayemdhulumu maskini ili kujiongezea mali,naye anayempa tajiri zawadi, wote huwa maskini.