Mithali1swh_onmm

1Mithali za Sulemani mwana wa Daudi, mfalme wa Israeli:2Kwa kupata hekima na nidhamu;kwa kufahamu maneno ya busara;3kwa kujipatia nidhamu na busara,kufanya lililo sawa, haki na bila kupendelea;4huwapa busara wajinga ,maarifa na akili kwa vijana;5wenye hekima na wasikilize nao waongeze elimu yao,wenye kupambanua na wapate mwongozo;6kwa kufahamu mithali na mifano,misemo na vitendawili vya wenye hekima.
7Kumcha Mwenyezi Mungu ni chanzo cha maarifa,lakini wapumbavu hudharau hekima na adabu.

Onyo dhidi ya ushawishi wa rafiki waovu

8Mwanangu, sikiliza mwongozo wa baba yako,wala usiyaache mafundisho ya mama yako.9Hayo yatakuwa taji la maua la neema kichwani pako,na mkufu wa kuipamba shingo yako.
10Mwanangu, wenye dhambi wakikushawishi,usikubaliane nao.11Wakisema, “Twende tufuatane;tukamvizie mtu na kumwaga damu,njoo tukavizie nafsi isiyo na hatia;12tuwameze wakiwa hai kama kaburi ,wakiwa wazima kama wale wanaotumbukia shimoni.13Tutapata aina zote za vitu vya thamanina kujaza nyumba zetu kwa nyara.14Njoo ushirikiane nasi,vitu vyote tutakavyopata tutagawana.”15Mwanangu, usiandamane nao.Usiweke mguu wako katika njia zao,16kwa kuwa miguu yao hukimbilia kwenye dhambi,ni wepesi kumwaga damu.17Tazama ni jinsi gani ilivyo kazi bure kutandaza wavuwakati ndege wote wanakuona!18Watu hawa huvizia kumwaga damu yao wenyewe;hujivizia tu wenyewe!19Huu ndio mwisho wa wote ambao wanajipatia mali kwa hila;huuondoa uhai wa wale wenye mali.

Onyo dhidi ya kukataa hekima

20Hekima huita kwa sauti kuu barabarani,hupaza sauti yake kwenye viwanja vikubwa;21kwenye makutano ya barabara za mjizenye makelele mengi hupaza sauti,kwenye malango ya mji hutoa hotuba yake:
22“Enyi wajinga, mtashikilia ujinga wenu hadi lini?Hadi lini wenye mizaha watafurahia mizaha,na wapumbavu kuchukia maarifa?23Kama mngekuwa mmeitikia karipio langu,ningekuwa nimemimina roho yangu kwenuna kuwafahamisha maneno yangu.24Lakini kwa kuwa mlinikataa nilipowaitana hakuna yeyote aliyekubaliniliponyoosha mkono wangu,25kwa kuwa mliyapuuza mashauri yangu yotena hamkukubali karipio langu,26mimi nami nitawacheka katika maafa yenu,nitawadhihaki janga litakapowapata:27janga litakapowapata kama tufani,maafa yatakapowazoa kama upepo wa kisulisuli,dhiki na taabu zitakapowalemea.
28“Ndipo watakaponiita lakini sitawajibu;watanitafuta lakini hawatanipata.29Kwa kuwa walichukia maarifa,wala hawakuchagua kumcha Mwenyezi Mungu,30kwa kuwa hawakukubali mashauri yangu,na kukataa maonyo yangu,31watakula matunda ya njia zao,na watashibishwa matunda ya hila zao.32Kwa kuwa ukaidi wa wajinga utawaua,na kuridhika kwa wajinga kutawaangamiza.33Lakini yeyote anisikilizaye ataishi kwa usalama,atatulia, bila kuwa na hofu ya madhara.”