Filemoni1
Salamu
1Paulo, mfungwa wa Al-Masihi Isa, pamoja na Timotheo ndugu yetu.Kwa Filemoni rafiki yetu mpendwa na mtendakazi mwenzetu,2kwa dada yetu mpendwa Afia, kwa Arkipo askari mwenzetu na kwa kundi la waumini wanaokutana nyumbani mwako.3Neema na amani zitokazo kwa Mungu, Baba yetu, na kwa Bwana wetu Isa Al-Masihi ziwe nanyi.