Hesabu24swh_onmm
1Basi Balaamu alipoona imempendeza Mwenyezi Mungu kubariki Israeli, hakuendelea tena kutafuta uchawi kama nyakati nyingine, bali aligeuza uso wake kuelekea nyikani.2Balaamu alipotazama nje na kuona Israeli amepiga kambi kabila kwa kabila, Roho wa Mungu akawa juu yake,3naye akatoa ujumbe wake:“Ujumbe wa Balaamu mwana wa Beori,ujumbe wake yeye ambaye jicho lake linaona vizuri;4ujumbe wake yeye anayesikia maneno ya Mungu,anayeona maono kutoka kwa Mwenyezi ,ambaye husujudu, na macho yake yamefunguka:5“Tazama jinsi yalivyo mazuri mahema yako, ee Yakobo,maskani zako, ee Israeli!6“Kama mabonde, yanaenea,kama bustani kando ya mto,kama miti ya udi iliyopandwa na Mwenyezi Mungu,kama mierezi kando ya maji.7Maji yatatiririka kutoka ndoo zake;mbegu yake itakuwa na maji tele.“Mfalme wake atakuwa mkuu kuliko Mfalme Agagi;ufalme wake utatukuka.8“Mungu alimleta kutoka Misri;yeye ana nguvu kama nyati.Anayararua mataifa yaliyo adui zake,na kuvunja mifupa yao vipande vipande;huwachoma kwa mishale yake.9Hujikunyata na kuvizia kama simba,kama simba jike; nani anayethubutu kumwamsha?“Abarikiwe kila akubarikiye,na alaaniwe kila akulaaniye!”10Ndipo hasira ya Balaki ikawaka dhidi ya Balaamu. Akapiga mikono yake pamoja, akamwambia Balaamu, “Nilikuita uje kuwalaani adui zangu, lakini umewabariki mara hizi tatu.11Sasa ondoka upesi uende nyumbani! Mimi nilisema nitakuzawadia vizuri sana, lakini Mwenyezi Mungu amekuzuia usizawadiwe.”12Balaamu akamwambia Balaki, “Je, hukumbuki jinsi nilivyowaambia wajumbe uliowatuma kwangu? Niliwaambia hivi,13‘Hata ikiwa Balaki angenipa jumba lake la kifalme likiwa limejazwa fedha na dhahabu, nisingeweza kufanya kitu chochote kwa matakwa yangu, kikiwa kizuri au kibaya, kwenda kinyume na agizo la Mwenyezi Mungu, nami imenipasa kusema tu kile Mwenyezi Mungu atakachosema’?14Sasa ninarudi kwa watu wangu. Lakini njoo, nikuonye kuhusu kile watu hawa watakachowatenda watu wako siku zijazo.”