Hesabu13swh_onmm
Kupeleleza Kanaani
1Mwenyezi Mungu akamwambia Musa,2“Watume baadhi ya watu wakaipeleleze nchi ya Kanaani, ninayowapa Waisraeli. Kutoka kwa kila kabila la baba zao, tuma mwanaume aliye mmoja wa viongozi wao.”3Hivyo kwa agizo la Mwenyezi Mungu Musa akawatuma kutoka Jangwa la Parani. Wote walikuwa viongozi wa Waisraeli.4Haya ndiyo majina yao:kutoka kabila la Reubeni, Shamua mwana wa Zakuri;5kutoka kabila la Simeoni, Shafati mwana wa Hori;6kutoka kabila la Yuda, Kalebu mwana wa Yefune;7kutoka kabila la Isakari, Igali mwana wa Yusufu;8kutoka kabila la Efraimu, Hoshea mwana wa Nuni;9kutoka kabila la Benyamini, Palti mwana wa Rafu;10kutoka kabila la Zabuloni, Gadieli mwana wa Sodi,11kutoka kabila la Manase (kabila la Yusufu), Gadi mwana wa Susi;12kutoka kabila la Dani, Amieli mwana wa Gemali;13kutoka kabila la Asheri, Sethuri mwana wa Mikaeli;14kutoka kabila la Naftali, Nabi mwana wa Wofsi;15kutoka kabila la Gadi, Geueli mwana wa Maki.16Haya ndiyo majina ya watu ambao Musa aliwatuma kuipeleleza nchi. (Musa akampa Hoshea mwana wa Nuni jina Yoshua.)17Musa alipowatuma wakaipeleleze Kanaani, alisema, “Pandeni kupitia Negebu, mwende hadi nchi ya vilima.18Mwone nchi ni ya namna gani, na kama watu wanaoishi humo wana nguvu au ni wadhaifu, iwapo ni wachache au wengi.19Wanaishi katika nchi ya namna gani? Je, ni nzuri au mbaya? Wanaishi katika miji ya namna gani? Je, haina kuta au ngome?20Ardhi ikoje? Ina rutuba au la? Je, kuna miti ndani yake au la? Jitahidini kadiri mnavyoweza kuleta baadhi ya matunda ya nchi.” (Ulikuwa msimu wa kuiva zabibu za kwanza.)21Hivyo wakapanda na kuipeleleza nchi kutoka Jangwa la Sini hadi Rehobu, kuelekea Lebo-Hamathi.22Wakapanda kupitia Negebu hadi wakafika Hebroni, mahali ambapo Ahimani, Sheshai na Talmai, wazao wa Anaki, waliishi. (Hebroni ulikuwa umejengwa miaka saba kabla ya mji wa Soani ulioko Misri.)23Walipofika katika Bonde la Eshkoli, walikata tawi lililokuwa na kishada kimoja cha zabibu. Wawili wao wakalichukua lile tawi kwenye mti, pamoja na komamanga na tini.24Eneo lile likaitwa Bonde la Eshkoli kwa sababu ya kile kishada cha zabibu ambacho Waisraeli walikikata huko.25Baada ya siku arobaini, wakarudi kutoka kuipeleleza nchi.