Nehemia12swh_onmm
Makuhani na Walawi waliorudi na Zerubabeli
1Wafuatao walikuwa makuhani na Walawi ambao walirudi na Zerubabeli mwana wa Shealtieli pamoja na Yeshua:Seraya, Yeremia, Ezra,2Amaria, Maluki, Hatushi,3Shekania, Rehumu, Meremothi,4Ido, Ginethoni, Abiya,5Miyamini, Moadia, Bilga,6Shemaya, Yoyaribu, Yedaya,7Salu, Amoki, Hilkia na Yedaya.
Hawa walikuwa viongozi wa makuhani na wenzao wakati wa Yeshua.8Walawi walikuwa Yeshua, Binui, Kadmieli, Sherebia, Yuda, na pia Matania, ambaye pamoja na wenzake, alikuwa kiongozi wa nyimbo za shukrani.9Bakbukia na Uni, wenzao, walisimama mkabala nao wakati wa ibada.10Yeshua alikuwa baba wa Yoyakimu, Yoyakimu alikuwa baba wa Eliashibu, Eliashibu alikuwa baba wa Yoyada,11Yoyada alikuwa baba wa Yonathani, na Yonathani alikuwa baba wa Yadua.12Katika siku za Yoyakimu, kulikuwa na wakuu wa jamaa za kikuhani:
wa jamaa ya Seraya, Meraya; wa jamaa ya Yeremia, Hanania;13wa jamaa ya Ezra, Meshulamu; wa jamaa ya Amaria, Yehohanani;14wa jamaa ya Maluki, Yonathani; wa jamaa ya Shebania, Yusufu;15wa jamaa ya Harimu, Adna; wa jamaa ya Meremothi, Helkai;16wa jamaa ya Ido, Zekaria; wa jamaa ya Ginethoni, Meshulamu;17wa jamaa ya Abiya, Zikri; wa jamaa ya Miyamini na ya Maazia, Piltai;18wa jamaa ya Bilgai, Shamua; wa jamaa ya Shemaya, Yehonathani;19wa jamaa ya Yoyaribu, Matenai; wa jamaa ya Yedaya, Uzi;20wa jamaa ya Salu, Kalai; wa jamaa ya Amoki, Eberi;21wa jamaa ya Hilkia, Hashabia; wa jamaa ya Yedaya, Nethaneli.22Wakuu wa jamaa za Walawi katika siku za Eliashibu, Yoyada, Yohanani na Yadua, pia wale jamaa za makuhani, waliandikishwa wakati wa utawala wa Dario Mwajemi.23Wakuu wa jamaa miongoni mwa wazao wa Lawi hadi wakati wa Yohanani mwana wa Eliashibu waliandikishwa katika kitabu cha kumbukumbu.24Viongozi wa Walawi walikuwa: Hashabia, Sherebia, Yeshua mwana wa Kadmieli na wenzao, waliosimama mkabala nao kusifu na kushukuru, sehemu moja ikipokezana na nyingine kama ilivyoagizwa na Daudi mtu wa Mungu.25Mabawabu waliokuwa wakilinda kwenye malango ya ghala ni: Matania, Bakbukia, Obadia, Meshulamu, Talmoni na Akubu.26Walihudumu siku za Yoyakimu mwana wa Yeshua, mwana wa Yosadaki, na katika siku za mtawala Nehemia, na za Ezra kuhani na mwandishi.