1Sikiliza asemalo Mwenyezi Mungu:“Simama, jitetee mbele ya milima;vilima na visikie lile unalotaka kusema.2“Sikilizeni, ee milima, mashtaka ya Mwenyezi Mungu,sikilizeni, enyi misingi ya milele ya dunia.Kwa kuwa Mwenyezi Mungu ana shauri dhidi ya watu wake;anatoa mashtaka dhidi ya Israeli.3“Watu wangu, nimewatendea nini?Nimewalemea kwa jinsi gani? Mnijibu.4Nimewatoa kutoka Misri na kuwakomboakutoka nchi ya utumwa.Nilimtuma Musa awaongoze,pia Haruni na Miriamu.5Watu wangu, kumbukeni jinsi Balaki mfalme wa Moabualivyofanya shaurina kile Balaamu mwana wa Beori alichojibu.Kumbukeni safari yenu kutoka Shitimu hadi Gilgali,ili mfahamu matendo ya haki ya Mwenyezi Mungu.”6Nimjie Mwenyezi Mungu na kitu gani na kusujudumbele za Mungu aliyetukuka?Je, nije mbele zake na sadaka za kuteketezwa,nije na ndama za mwaka mmoja?7Je, Mwenyezi Mungu atafurahishwa na kondoo dume elfu,au mito elfu kumi ya mafuta?Je, nimtoe mzaliwa wangu wa kwanzakwa ajili ya kosa langu,mtoto wangu mwenyewekwa ajili ya dhambi ya nafsi yangu?8Amekuonesha yaliyo mema, ee mwanadamu.Mwenyezi Mungu anataka nini kwako?Ila kutenda kwa haki na kupenda rehema,na kwenda kwa unyenyekevu na Mungu wako.
Hatia na adhabu ya Israeli
9Sikiliza! Mwenyezi Mungu anauita mji:kulicha jina lako ni hekima:“Tii hiyo fimbo na yeye aliyeiamuru.10Je, bado nisahau, ee nyumba ya uovu,hazina yako uliyopata kwa udanganyifuna vipimo vilivyopunguka,ambavyo vimelaaniwa?11Je, naweza kuhukumu kuwamtu mwenye mizani ya udanganyifu hana hatia,aliye na mfuko wa mawe ya kupimia ya uongo?12Matajiri wake ni wajeuri;watu wake ni waongona ndimi zao zinazungumzakwa udanganyifu.13Kwa hiyo, nimeanza kukuharibu,kuwaangamiza kwa sababu ya dhambi zenu.14Mtakula lakini hamtashiba;tumbo zenu bado zitakuwa tupu.Mtaweka akiba lakini hamtaokoa chochote,kwa sababu mtakachoweka akibanitatoa kwa upanga.15Mtapanda lakini hamtavuna;mtakamua zeituni lakinihamtatumia mafuta yake.Mtakamua zabibulakini hamtakunywa hiyo divai.16Mmezishika sheria za Omrina matendo yote ya nyumba ya Ahabu,tena umefuata desturi zao.Kwa hiyo nitakutoa kwa maangamizina watu wako kuwa dhihaka;mtachukua dharau za mataifa.”