1Katika siku za mwishomlima wa Hekalu la Mwenyezi Mungu utaimarishwakama mlima mkuu miongoni mwa milima yote;utainuliwa juu ya vilima,na watu wa mataifa watamiminika humo.2Mataifa mengi yatakuja na kusema,“Njooni, twendeni kwenye mlima wa Mwenyezi Mungu,kwenye nyumba ya Mungu wa Yakobo.Atatufundisha njia zake,ili tuweze kuenenda katika mapito yake.”Torati itatoka Sayuni,neno la Mwenyezi Mungu litatoka Yerusalemu.3Atahukumu kati ya mataifa mengi,na ataamua migogoro ya mataifayenye nguvu na yaliyo mbali.Watafua panga zao ziwe majembe,na mikuki yao kuwa miundu ya kukata matawi.Taifa halitainua upanga dhidi ya taifa jingine,wala hawatajifunza vita tena.4Kila mtu ataketi chini ya mzabibu wakena chini ya mtini wake,wala hakuna mtu atakayewaogopesha,kwa kuwa Mwenyezi Mungu,Mungu wa majeshi ya mbinguni amesema.5Mataifa yote yanaweza kutembeakatika jina la miungu yao;sisi tutatembea katika jina la Mwenyezi Mungu,Mungu wetu milele na milele.
Mpango wa Mwenyezi Mungu
6“Katika siku hiyo,” asema Mwenyezi Mungu,“nitawakusanya walemavu;nitawakusanya walio uhamishonina wale niliowahuzunisha.7Nitawafanya walemavu kuwa mabaki,wale waliofukuzwa kuwa taifa lenye nguvu.Mwenyezi Mungu atawatawala katika Mlima Sayunikuanzia siku hiyo na hata milele.8Lakini kwako wewe, ee mnara wa ulinzi wa kundi,ee ngome ya Binti Sayuni,milki ya awali itarudishwa kwako,ufalme utakuja kwa Binti Yerusalemu.”9Kwa nini sasa unalia kwa nguvu:kwani huna mfalme?Je, mshauri wako amekufa, hata maumivu yakukamatekama ya mwanamkealiye na uchungu wa kuzaa?10Gaagaa kwa uchungu, ee Binti Sayuni,kama mwanamke mwenye uchungu wa kuzaa,kwa kuwa sasa ni lazima uuache mjiukapige kambi uwanjani.Utaenda Babeli;huko utaokolewa.Huko Mwenyezi Mungu atakukomboakutoka mikononi mwa adui zako.11Lakini sasa mataifa mengiyamekusanyika dhidi yako.Wanasema, “Mwache anajisiwe,macho yetu na yatazame Sayuni kwa furaha!”12Lakini hawayajuimawazo ya Mwenyezi Mungu;hawauelewi mpango wake,yeye awakusanyaye kama migandakwenye sakafu ya kupuria.13“Inuka upure, ee Binti Sayuni,kwa kuwa nitakupa pembe za chuma;nitakupa kwato za shabana utavunja vipande vipande mataifa mengi.”Utatoa mapato yao waliopata kwa udanganyifu kwa Mwenyezi Mungu,utajiri wao kwa Bwana wa dunia yote.