Mika1swh_onmm
1Neno la Mwenyezi Mungu lilimjia Mika Mmoreshethi wakati wa utawala wa Yothamu, Ahazi na Hezekia, wafalme wa Yuda, ufunuo aliouona kuhusu Samaria na Yerusalemu.2Sikieni, enyi mataifa, enyi nyote,sikilizeni, ee dunia na wote mliomo,ili Bwana Mungu Mwenyezi ashuhudie dhidi yenu,Bwana kutoka Hekalu lake takatifu.