Mathayo10swh_onmm
Isa achagua mitume kumi na wawili
1Ndipo Isa akawaita wanafunzi wake kumi na wawili, naye akawapa mamlaka juu ya pepo wachafu, ili waweze kuwatoa na kuponya kila ugonjwa na maradhi ya kila aina.2Haya ndiyo majina ya hao mitume kumi na wawili:wa kwanza, Simoni aitwaye Petro, na Andrea nduguye; Yakobo mwana wa Zebedayo, na Yohana nduguye;3Filipo, na Bartholomayo; Tomaso, na Mathayo mtoza ushuru; Yakobo mwana wa Alfayo, na Thadayo;4Simoni Mkananayo, na Yuda Iskariote aliyemsaliti Isa.