Mathayo1swh_onmm
Kumbukumbu za ukoo wa Isa Al-Masihi
1Habari za ukoo wa Isa Al-Masihi mwana wa Daudi, mwana wa Ibrahimu:2Ibrahimu akamzaa Isaka, Isaka akamzaa Yakobo, Yakobo akawazaa Yuda na ndugu zake,3Yuda akawazaa Peresi na Zera, ambao mama yao alikuwa Tamari, Peresi akamzaa Esromu, Esromu akamzaa Aramu,4Aramu akamzaa Aminadabu, Aminadabu akamzaa Nashoni, Nashoni akamzaa Salmoni,5Salmoni akamzaa Boazi, na mama yake Boazi alikuwa Rahabu, Boazi akamzaa Obedi, ambaye mama yake alikuwa Ruthu, Obedi akamzaa Yese,6Yese akamzaa Daudi, aliyekuwa mfalme.Daudi akamzaa Sulemani, ambaye mama yake ni yule aliyekuwa mke wa Uria.7Sulemani akamzaa Rehoboamu, Rehoboamu akamzaa Abiya, Abiya akamzaa Asa,8Asa akamzaa Yehoshafati, Yehoshafati akamzaa Yoramu, Yoramu akamzaa Uzia,9Uzia akamzaa Yothamu, Yothamu akamzaa Ahazi, Ahazi akamzaa Hezekia,10Hezekia akamzaa Manase, Manase akamzaa Amoni, Amoni akamzaa Yosia,11wakati wa uhamisho wa Babeli, Yosia alimzaa Yekonia na ndugu zake.12Baada ya uhamisho wa Babeli: Yekonia alimzaa Shealtieli, Shealtieli akamzaa Zerubabeli,13Zerubabeli akamzaa Abihudi, Abihudi akamzaa Eliakimu, Eliakimu akamzaa Azori,14Azori akamzaa Sadoki, Sadoki akamzaa Akimu, Akimu akamzaa Eliudi,15Eliudi akamzaa Eleazari, Eleazari akamzaa Matani, Matani akamzaa Yakobo,16naye Yakobo akamzaa Yusufu, aliyekuwa mumewe Mariamu, mama yake Isa, aitwaye Al-Masihi.17Hivyo, kulikuwa na jumla ya vizazi kumi na vinne tangu Ibrahimu hadi Daudi, vizazi kumi na vinne tangu Daudi hadi wakati wa uhamisho wa Babeli, na vizazi kumi na vinne tangu wakati wa uhamisho wa Babeli hadi Al-Masihi.