Marko3swh_onmm
Isa amponya mtu aliyepooza mkono
1Isa akaingia tena ndani ya sinagogi, na kulikuwa na mtu aliyepooza mkono.2Wakawa wanamwangalia waone kama atamponya huyo mtu siku ya Sabato, ili wapate sababu ya kumshtaki.3Isa akamwambia yule mtu mwenye mkono uliopooza, “Njoo hapa mbele ya watu wote.”4Kisha Isa akawauliza, “Je, ni lipi lililo halali siku ya Sabato: Ni kutenda mema au kutenda mabaya? Ni kuokoa maisha au kuua?” Lakini wao wakanyamaza.5Isa akawatazama kwa hasira watu waliomzunguka pande zote, akahuzunika sana kwa sababu ya ugumu wa mioyo yao. Akamwambia yule mtu mwenye mkono uliopooza, “Nyoosha mkono wako.” Akaunyoosha, nao ukawa umeponywa kabisa!6Kisha Mafarisayo wakatoka nje, nao wakaanza kufanya njama ya kumuua Isa wakishirikiana na Maherode.Makundi ya watu wamfuata Isa
7Isa na wanafunzi wake wakaondoka huko, wakaenda baharini, nao umati mkubwa wa watu kutoka Galilaya wakamfuata.8Waliposikia mambo yote aliyokuwa akiyafanya, makundi ya watu wakamjia kutoka Yudea, Yerusalemu, Idumaya, na ng’ambo ya Yordani, pamoja na wale wa maeneo ya Tiro na Sidoni.9Kwa sababu ya umati mkubwa wa watu, aliwaambia wanafunzi wake watayarishe mashua ndogo kwa ajili yake, ili kuwazuia watu kumsonga.10Kwa kuwa alikuwa amewaponya wagonjwa wengi, wale wenye magonjwa walikuwa wanasukumana ili wapate kumgusa.11Kila mara pepo wachafu walipomwona, walianguka chini mbele yake na kupiga kelele wakisema, “Wewe ndiwe Mwana wa Mungu.”12Lakini aliwaonya wasiwaambie wengine kumhusu.Isa achagua mitume kumi na wawili
13Isa akapanda mlimani na kuwaita wale aliowataka, nao wakamjia.14Akawachagua watu kumi na wawili ambao aliwaita mitume, ili wapate kuwa naye, na awatume kwenda kuhubiri15na kuwa na mamlaka ya kutoa pepo wachafu.16Hawa ndio wale kumi na wawili aliowachagua:Simoni (ambaye alimwita Petro);17Yakobo mwana wa Zebedayo, na Yohana nduguye (ambao aliwaita Boanerge, maana yake Wana wa Ngurumo);18Andrea, Filipo, Bartholomayo, Mathayo, Tomaso, Yakobo mwana wa Alfayo, Thadayo, Simoni Mkananayo,19na Yuda Iskariote aliyemsaliti Isa.