Maombolezo4swh_onmm

1Jinsi dhahabu ilivyopoteza mng’ao wake,dhahabu iliyo safi haing’ai!Vito vya thamani vimetawanywakwenye mwanzo wa kila barabara.
2Wana wa Sayuni wenye thamani,ambao mwanzo uzito wa thamani yaoulikuwa wa dhahabu,sasa wanaangaliwa kama vyungu vya udongo,kazi ya mikono ya mfinyanzi!
3Hata mbweha hutoa matiti yaokunyonyesha watoto wao,lakini watu wangu wamekuwa wasio na hurumakama mbuni jangwani.
4Kwa sababu ya kiu ulimi wa mtoto mchangaumegandamana na kaakaa la kinywa chake,watoto huomba mkate,lakini hakuna yeyote awapaye.
5Wale waliokula vyakula vya kifaharini maskini barabarani.Wale waliokuzwa wakivaa nguo za zambarausasa wanalalia majivu.
6Adhabu ya watu wanguni kubwa kuliko ile ya Sodoma,ambayo ilipinduliwa ghafulawala hapakuwa na mkono wa msaada.
7Wakuu wao walikuwa wameng’aa kuliko thelujina weupe kuliko maziwa,miili yao ilikuwa myekundu kuliko marijani,kuonekana kwao kama yakuti samawi.
8Lakini sasa ni weusi kuliko masizi;hawatambulikani barabarani.Ngozi yao imeshikamana juu ya mifupa yao,imekuwa mikavu kama fimbo.
9Wale waliouawa kwa upanga ni borakuliko wale wanaokufa njaa;wanateseka kwa njaa, wanatokomeakwa kukosa chakula kutoka shambani.
10Kwa mikono yao wenyewe wanawake wenye hurumawanapika watoto wao wenyewe,waliokuwa chakula chaowatu wangu walipoangamizwa.
11Mwenyezi Mungu ametoa nafasi kamilifu ya ghadhabu yake;ameimwaga hasira yake kali.Amewasha moto katika Sayuniambao umeteketeza misingi yake.
12Wafalme wa dunia hawakuamini,wala mtu yeyote wa duniani,kwamba adui na watesi wangeweza kuingiakwenye malango ya Yerusalemu.
13Lakini hili lilitokea kwa sababu ya dhambi za manabii wake,na maovu ya makuhani wake,waliomwaga ndani yakedamu ya wenye haki.
14Sasa wanapapasa papasa barabaranikama watu ambao ni vipofu.Wamenajisiwa kabisa kwa damu,hata hakuna anayethubutu kugusa mavazi yao.
15Watu wanawapigia kelele, “Ondokeni! Ninyi ni najisi!Ondokeni! Ondokeni! Msituguse!”Wanapokimbia na kutangatanga,watu miongoni mwa mataifa wanasema,“Hawawezi kukaa hapa zaidi.”
16Mwenyezi Mungu mwenyewe amewatawanya;hawaangalii tena.Makuhani hawaoneshwi heshima,wazee hawakubaliki.
17Zaidi ya hayo, macho yetu yalichoka,kwa kutazamia bure msaada;tuliangalia kutoka minara yetukwa taifa lisiloweza kutuokoa.
18Watu walituvizia katika kila hatuahata hatukuweza kutembea katika barabara zetu.Mwisho wetu ulikuwa karibu, siku zetu zilikuwa zimetimia,kwa maana mwisho wetu ulikuwa umefika.
19Waliotufuatia walikuwa wepesikuliko tai angani;walitusaka juu milimanina kutuvizia jangwani.
20Mpakwa mafuta wa Mwenyezi Mungu, pumzi ya uhai wetu hasa,alinaswa katika mitego yao.Tulifikiri kwamba chini ya kivuli chaketungeishi miongoni mwa mataifa.
21Shangilia na ufurahi, ee Binti Edomu,wewe unayeishi nchi ya Usi.Lakini kwako pia kikombe kitapitishwa,Utalewa na kuvuliwa nguo ubaki uchi.
22Ee Binti Sayuni, adhabu yako itaisha,hatarefusha muda wako wa kukaa uhamishoni.Lakini, ee Binti Edomu, ataadhibu dhambi yako,na atafunua uovu wako.