Maombolezo3swh_onmm
1Mimi ndiye mtu aliyeona matesokwa fimbo ya ghadhabu yake.2Amenifukuzia mbali na kunifanya nitembeegizani wala si katika nuru;3hakika, amegeuza mkono wake dhidi yangutena na tena, mchana kutwa.4Amefanya ngozi yangu na nyama yangu kuchakaana ameivunja mifupa yangu.5Amenizingira na kunizungukakwa uchungu na taabu.6Amenifanya niishi gizanikama wale waliokufa.7Amenizungushia ukuta ili nisiweze kutoroka,amenifunga kwa minyororo mizito.8Hata ninapoita au kulia ili kuomba msaada,anakataa kupokea maombi yangu.9Ameizuia njia yangu kwa mapande ya mawe,amepotosha njia zangu.10Kama dubu aviziaye,kama simba mafichoni,11ameniburuta kutoka njiani,akanirarua na kuniacha bila msaada.12Amevuta upinde wakena kunifanya mimi niwe lengo kwa ajili ya mishale yake.13Alinichoma moyo wangu kwa mishaleiliyotoka kwenye podo lake.14Nimekuwa kichekesho kwa watu wangu wote,wananidhihaki kwa wimbo mchana kutwa.15Amenijaza kwa majani machunguna kunishibisha kwa nyongo.16Amevunja meno yangu kwa changarawe,amenikanyagia mavumbini.17Amani yangu imeondolewa,nimesahau kufanikiwa ni nini.18Kwa hiyo nasema, “Fahari yangu imeondokana yale yote niliyokuwa nimetarajia kutoka kwa Mwenyezi Mungu.”19Nayakumbuka mateso yangu na kutangatanga kwangu,uchungu na nyongo.20Ninayakumbuka vyema,nayo nafsi yangu imezimia ndani yangu.21Hata hivyo najikumbusha neno hilina kwa hiyo ninalo tumaini.22Kwa sababu ya upendo mkuu wa Mwenyezi Mungu, hatuangamii,kwa kuwa huruma zake hazikomi kamwe.23Ni mpya kila asubuhi,uaminifu wako ni mkuu.24Nimeiambia nafsi yangu, “Mwenyezi Mungu ni fungu langu,kwa hiyo nitamngojea.”25Mwenyezi Mungu ni mwema kwa wale wanaomtumaini,na kwa yule anayemtafuta;26ni vyema kungojea kwa utulivukwa ajili ya wokovu wa Mwenyezi Mungu.27Ni vyema mtu kuchukua nirabado angali kijana.28Na akae peke yake awe kimya,kwa maana Mwenyezi Mungu ameiweka juu yake.29Hata azike uso wake mavumbinibado tumaini litakuwepo.30Na atoe shavu lake kwa yule ampigaye,na ajazwe na aibu.31Kwa kuwa watu hawakatiliwi mbalina Bwana milele.32Ingawa huleta huzuni, ataonesha huruma,kwa kuwa upendo wake usiokoma ni mkuu.33Kwa maana hapendi kuwaletea matesoau huzuni watoto wa wanadamu.34Kuwaponda chini ya nyayowafungwa wote katika nchi,35Kumnyima mtu haki zakembele za Aliye Juu Sana,36kumnyima mtu haki:Je, Bwana asione mambo kama haya?37Nani awezaye kusema nalo likatendekakama Bwana hajaamuru?38Je, si ni kwenye kinywa cha Aliye Juu Sanandiko yatokako maafa na mambo mema?39Je, mwanadamu yeyote aliye hai aweza kulalamikawakati anapoadhibiwa kwa ajili ya dhambi zake?40Tuzichunguze njia zetu na kuzijaribu,na tumrudie Mwenyezi Mungu.41Tuinue mioyo yetu pamoja na mikono yetukwa Mungu mbinguni, na tuseme:42“Tumetenda dhambi na kuasinawe hujasamehe.43“Umejifunika mwenyewe kwa hasira na kutufuatilia;umetuchinja bila huruma.44Unajifunika mwenyewe kwa wingu,ili pasiwe na ombilitakaloweza kupenya.45Umetufanya takataka na uchafumiongoni mwa mataifa.46“Adui zetu wote wamefumbua vinywa vyaowazi dhidi yetu.47Tumeteseka kwa hofu kuu na shida ya ghafula,uharibifu na maangamizi.”48Vijito vya machozi vinatiririka kutoka machoni mwangu,kwa sababu watu wangu wameangamizwa.49Macho yangu yatatiririka machozi bila kukoma,bila kupata nafuu,50hadi Mwenyezi Mungu atazame chinikutoka mbinguni na kuona.51Lile ninaloliona huniletea huzuni nafsinikwa sababu ya wanawake wote wa mji wangu.52Wale waliokuwa adui zangu bila sababuwameniwinda kama ndege.53Walijaribu kukomesha maisha yangu ndani ya shimona kunitupia mawe;54maji yalifunika juu ya kichwa changu,nami nikafikiri nilikuwa karibukukatiliwa mbali.55Nililiitia jina lako, Ee Mwenyezi Mungu,kutoka vina vya shimo.56Ulisikia ombi langu: “Usikizibie masikio yakokilio changu nikuombapo msaada.”57Ulikuja karibu nilipokuita,nawe ukasema, “Usiogope.”58Ee Bwana, ulichukua shauri langu,ukaukomboa uhai wangu.59Umeona, Ee Mwenyezi Mungu, ubaya niliotendewa.Tetea shauri langu!60Umeona kina cha kisasi chao,mashauri yao yote mabaya dhidi yangu.61Ee Mwenyezi Mungu, umesikia matukano yao,mashauri yao yote mabaya dhidi yangu:62kile adui zangu wanachonong’ona na kunung’unikiadhidi yangu mchana kutwa.63Watazame! Wakiwa wameketi au wamesimama,wananidhihaki katika nyimbo zao.64Uwalipe kile wanachostahili, Ee Mwenyezi Mungu,kwa yale ambayo mikono yao imetenda.65Weka pazia juu ya mioyo yao,laana yako na iwe juu yao!66Wafuatilie katika hasira na uwaangamizechini ya mbingu za Mwenyezi Mungu.