Maombolezo2swh_onmm

1Tazama jinsi Bwana alivyomfunika Binti Sayunikwa wingu la hasira yake!Ameitupa chini fahari ya Israelikutoka mbinguni hadi duniani,hakukumbuka kiti chake cha kuwekea miguukatika siku ya hasira yake.
2Bila huruma Bwana ameyamezamakao yote ya Yakobo;katika ghadhabu yake amebomoangome za Binti Yuda.Ameuangusha ufalme wake na wakuu wakechini kwa aibu.
3Katika hasira kali amevunjakila pembe ya Israeli.Ameuondoa mkono wake wa kuumealipokaribia adui.Amemteketeza Yakobo kama moto uwakaoule uteketezao kila kitu kinachouzunguka.
4Ameupinda upinde wake kama adui,mkono wake wa kuume uko tayari.Kama vile adui amewauawote waliokuwa wanapendeza jicho,amemwaga ghadhabu yake kama motojuu ya hema la Binti Sayuni.
5Bwana ni kama adui;amemmeza Israeli.Ameyameza majumba yake yote ya kifalmena kuangamiza ngome zake.Ameongeza huzuni na maombolezokwa Binti Yuda.
6Ameharibu maskani yake kama bustani,ameharibu mahali pake pa mkutano.Mwenyezi Mungu amemfanya Sayuni kusahausikukuu zake zilizoamriwa na Sabato zake;katika hasira yake kali amewadharaumfalme na kuhani.
7Bwana amekataa madhabahu yakena kuacha mahali patakatifu pake.Amemkabidhi adui kutaza majumba yake ya kifalme;wameshangilia katika nyumba ya Mwenyezi Mungukama katika siku ya sikukuu iliyoamriwa.
8Mwenyezi Mungu alikusudia kuangushaukuta uliomzunguka Binti Sayuni.Ameinyoosha kamba ya kupimiana hakuuzuia mkono wake usiangamize.Alifanya maboma na kuta ziomboleze,vyote vikaharibika pamoja.
9Malango yake yamezama ardhini,makomeo yake ameyavunja na kuyaharibu.Mfalme wake na wakuu wake wamepelekwa uhamishonimiongoni mwa mataifa,sheria haipo tena,na manabii wake hawapati tenamaono kutoka kwa Mwenyezi Mungu.
10Wazee wa Binti Sayuniwanaketi chini kimya,wamenyunyiza mavumbi kwenye vichwa vyaona kuvaa gunia.Wanawali wa Yerusalemuwameinamisha vichwa vyao hadi chini.
11Macho yangu yamedhoofika kwa kulia,nina maumivu makali ndani,moyo wangu umemiminwa ardhinikwa sababu watu wangu wameangamizwa,kwa sababu watoto na wanyonyao wanazimiakwenye barabara za mji.
12Wanawaambia mama zao,“Wapi mkate na divai?”wazimiapo kama watu waliojeruhiwakatika barabara za mji,maisha yao yadhoofikavyomikononi mwa mama zao.
13Ninaweza kusema nini kwa ajili yako?Nikulinganishe na nini,ee Binti Yerusalemu?Nitakufananisha na nini,ili nipate kukufariji,ee Bikira Binti Sayuni?Jeraha lako lina kina kama bahari.Ni nani awezaye kukuponya?
14Maono ya manabii wakoyalikuwa ya uongo na yasiyofaa kitu,hawakuifunua dhambi yakoili kukuzuilia kwenda utumwani.Maneno waliyokupayalikuwa ya uongo na ya kupotosha.
15Wote wapitiao njia yakowanakupigia makofi,wanakudhihaki na kutikisa vichwa vyaokwa Binti Yerusalemu:“Huu ndio ule mji ulioitwamkamilifu wa uzuri,furaha ya dunia yote?”
16Adui zako wote wanapanuavinywa vyao dhidi yako,wanadhihaki na kusaga meno yaona kusema, “Tumemmeza.Hii ndiyo siku tuliyoingojea,tumeishi na kuiona.”
17Mwenyezi Mungu amefanya lile alilolipanga;ametimiza neno lakealiloliamuru siku za kale.Amekuangusha bila huruma,amewaacha adui wakusimange,ametukuza pembe ya adui yako.
18Mioyo ya watuinamlilia Bwana.Ee ukuta wa Binti Sayuni,machozi yako na yatiririke kama mtousiku na mchana;usijipe nafuu,macho yako yasipumzike.
19Inuka, lia usiku,zamu za usiku zianzapo;mimina moyo wako kama majimbele za Bwana.Mwinulie yeye mikono yakokwa ajili ya maisha ya watoto wako,ambao wanazimia kwa njaakwenye kila mwanzo wa barabara.
20“Tazama, Ee Mwenyezi Mungu, ufikirie:Ni nani ambaye umepata kumtendea namna hii?Je, wanawake wale wazao wao,watoto waliowalea?Je, kuhani na nabii auawemahali patakatifu pa Bwana?
21“Vijana na wazee hujilaza pamojakatika mavumbi ya barabarani,wasichana wangu na wavulana wanguwameanguka kwa upanga.Umewaua katika siku ya hasira yako,umewachinja bila huruma.
22“Kama ulivyoita siku ya karamu,ndivyo ulivyoagiza mapigo dhidi yangu kila upande.Katika siku ya hasira ya Mwenyezi Munguhakuna yeyote aliyekwepa au kupona;wale niliowatunza na kuwalea,adui yangu amewaangamiza.”