Maombolezo1swh_onmm

1Tazama jinsi mji ulivyoachwa ukiwa,mji ambao zamani ulikuwa umejaa watu!Jinsi umekuwa kama mama mjane,ambaye wakati fulani alikuwa maarufu miongoni mwa mataifa!Yule aliyekuwa malkia miongoni mwa majimbosasa amekuwa mtumwa.
2Kwa uchungu, hulia sana usiku,machozi yapo kwenye mashavu yake.Miongoni mwa wapenzi wake wotehakuna yeyote wa kumfariji.Rafiki zake wote wamemsaliti,wamekuwa adui zake.
3Baada ya mateso na kufanyishwa kazi kikatili,Yuda ameenda uhamishoni.Anakaa miongoni mwa mataifa,hapati mahali pa kupumzika.Wote ambao wanamsaka wamemkamatakatikati ya dhiki yake.
4Barabara zielekeazo Sayuni zaomboleza,kwa kuwa hakuna yeyote anayekujakwenye sikukuu zake zilizoamriwa.Malango yake yote yamekuwa ukiwa,makuhani wake wanalia kwa uchungu,wanawali wake wanahuzunika,naye yuko katika uchungu wa maumivu makuu.
5Adui zake wamekuwa mabwana zake,watesi wake wana amani.Mwenyezi Mungu amemletea huzunikwa sababu ya dhambi zake nyingi.Watoto wake wameenda uhamishoni,wamekuwa mateka mbele ya adui.
6Fahari zilizokuwa zake zimeondokakutoka kwa Binti Sayuni.Wakuu wake wako kama ayalaambaye hapati malisho,wakiwa dhaifu wamekimbiambele ya aliyewakimbiza.
7Katika siku za mateso yake na kutangatanga,Yerusalemu hukumbuka hazina zoteambazo zilikuwa zake siku za kale.Watu wake walipoanguka katika mikono ya adui,hapatakuwa na yeyote wa kumsaidia.Watesi wake walimtazamana kumcheka katika maangamizi yake.
8Yerusalemu ametenda dhambi sanakwa hiyo amekuwa najisi.Wote waliomheshimu wanamdharau,kwa maana wameuona uchi wake.Yeye mwenyewe anapiga kitena kugeukia mbali.
9Uchafu wake umegandamana na nguo zake;hakuwaza juu ya maisha yake ya baadaye.Anguko lake lilikuwa la kushangaza,hapakuwa na yeyote wa kumfariji.“Tazama, Ee Mwenyezi Mungu, teso langu,kwa maana adui ameshinda.”
10Adui ametia mikonojuu ya hazina zake zote,aliona mataifa ya kipaganiwakiingia mahali patakatifu pake,wale uliowakataza kuingiakwenye kusanyiko lako.
11Watu wake wote wanalia kwa uchunguwatafutapo chakula;wanabadilisha hazina zao kwa chakulaili waweze kuendelea kuishi.“Tazama, Ee Mwenyezi Mungu, uangalie;kwa maana nimedharauliwa.”
12“Je, si kitu kwenu, ninyi nyote mpitao kando?Angalieni kote mwone.Je, kuna maumivu kama maumivu yanguyale yaliyotiwa juu yangu,yale Mwenyezi Mungu aliyoyaleta juu yangukatika siku ya hasira yake kali?
13“Kutoka juu alipeleka moto,akaushusha katika mifupa yangu.Aliitandia wavu miguu yanguna akanirudisha nyuma.Akanifanya mkiwa,na mdhaifu mchana kutwa.
14“Dhambi zangu zimefungwa kwenye nira,kwa mikono yake zilifumwa pamoja.Zimefika shingoni mwanguna Bwana ameziondoa nguvu zangu.Amenitia mikononi mwa waleambao siwezi kushindana nao.
15“Bwana amewakataa mashujaawote walio kati yangu;ameagiza jeshi dhidi yangukuwaponda vijana wangu.Katika shinikizo lake la kukamulia zabibuBwana amemkanyaga Bikira Binti Yuda.
16“Hii ndiyo sababu ninaliana macho yangu yanafurika machozi.Hakuna yeyote aliye karibu kunifariji,hakuna yeyote wa kuhuisha roho yangu.Watoto wangu ni wakiwakwa sababu adui ameshinda.”
17Sayuni ananyoosha mikono yake,lakini hakuna yeyote wa kumfariji.Mwenyezi Mungu ametoa amri kwa ajili ya Yakobokwamba majirani zake wawe adui zake;Yerusalemu umekuwakitu najisi miongoni mwao.
18“Mwenyezi Mungu ni mwenye haki,hata hivyo niliasi dhidi ya amri yake.Sikilizeni, enyi mataifa yote,tazameni maumivu yangu.Wasichana wangu na wavulana wanguwameenda uhamishoni.
19“Niliita washirika wangulakini walinisaliti.Makuhani wangu na wazee wanguwaliangamia mjiniwalipokuwa wakitafuta chakulaili waweze kuishi.
20“Angalia, Ee Mwenyezi Mungu, jinsi nilivyo katika dhiki!Nina maumivu makali ndani yangu,nami ninahangaika moyoni mwangu,kwa kuwa nimekuwa mwasi sana.Huko nje, upanga unaua watu,ndani, kipo kifo tu.
21“Watu wamesikia ninavyolia kwa uchungu,lakini hakuna yeyote wa kunifariji.Adui zangu wote wamesikia kuhusu dhiki yangu,wanafurahia lile ulilolitenda.Naomba uilete siku uliyoitangazaili wawe kama mimi.
22“Uovu wao wote na uje mbele zako;uwaadhibu vikalikama ulivyoniadhibukwa sababu ya dhambi zangu zote.Kulia kwangu kwa uchungu ni kwingina moyo wangu umedhoofika.”