1Siku hiyo Debora na Baraka mwana wa Abinoamu wakaimba wimbo huu:2“Wakuu katika Israeli wanapoongoza,wakati watu wanapojitoakwa hiari yao wenyewe:mhimidini Mwenyezi Mungu!3“Sikieni hili, enyi wafalme!Sikilizeni, enyi watawala!Nitamwimbia Mwenyezi Mungu, nitaimba;kwa wimbo nitamhimidi Mwenyezi Mungu,Mungu wa Israeli.4“Ee Mwenyezi Mungu, ulipotoka katika Seiri,ulipopita katika mashamba ya Edomu,nchi ilitetemeka, mbingu nazo zikamwaga,naam, mawingu yakamwaga maji.5Milima ilitetemeka mbele za Mwenyezi Mungu, Yule wa Sinai,mbele za Mwenyezi Mungu, Mungu wa Israeli.6“Katika siku za Shamgari mwana wa Anathi,katika siku za Yaeli,barabara kuu hazikuwa na watu;wasafiri walipita njia za kando.7Mashujaa walikoma katika Israeli,walikoma hadi mimi, Debora, nilipoinuka,nilipoinuka kama mama katika Israeli.8Mungu alichagua viongozi wapyavita vilipokuja malangoni ya mji;lakini hapakuonekana ngao wala mkukimiongoni mwa watu elfu arobaini katika Israeli.9Moyo wangu u pamoja na wakuu wa Israeli,u pamoja na wale wanaojitoa kwa hiari yaomiongoni mwa watu.Mhimidini Mwenyezi Mungu!10“Ninyi mpandao punda weupe,mkiketi juu ya matandiko ya thamani,nanyi mnaotembea barabarani,fikirini11kuhusu sauti za waimbajimahali pa kunyweshea maji.Wanasimulia matendo ya haki ya Mwenyezi Mungu,matendo ya haki ya mashujaa wakekatika Israeli.“Ndipo watu wa Mwenyezi Munguwalipoteremka malangoni pa mji.12‘Amka, amka! Debora!Amka, amka, uimbe!Ee Baraka! Inuka,chukua mateka wako uliowateka,ee mwana wa Abinoamu.’13“Ndipo mabaki ya watuwakashuka dhidi ya wakuu,watu wa Mwenyezi Mungu wakashuka kwangudhidi ya wenye nguvu.14Baadhi yao walitoka Efraimu,ambao chimbuko lao ni Amaleki;Benyamini alikuwa miongonimwa watu waliokufuata.Kutoka Makiri wakashuka viongozi,na kutoka Zabuloni wale washikaofimbo ya jemadari.15Wakuu wa Isakari walikuwa pamoja na Debora;naam, Isakari alikuwa pamoja na Baraka,wakija nyuma yake kwa mbiowakielekea bondeni.Katika jamaa za Reubeni,palikuwa na kujihoji kukubwa moyoni.16Kwa nini ulikaa katikati ya mazizi ya kondookusikiliza sauti ya filimbi zinazoita makundi?Kwa jamaa za Reubeni,palikuwa na kujihoji kukubwa moyoni.17Gileadi alikaa ng’ambo ya Yordani.Naye Dani, kwa nini alikaakwenye merikebu siku nyingi?Asheri alikaa kwa utulivu ufuoni mwa bahari,akikaa kwenye ghuba zake ndogo.18Watu wa Zabuloni walihatarisha maisha yao,vilevile nao watu wa Naftali.19“Wafalme walikuja na kufanya vita;wafalme wa Kanaani walipiganahuko Taanaki, karibu na maji ya Megido,lakini hawakuchukua nyara za fedha.20Kutoka mbinguni nyota zilipigana,nyota kutoka njia zakezilipigana na Sisera.21Mto wa Kishoni uliwasomba,ule mto wa zamani, mto wa Kishoni.Songa mbele, ee nafsi yangu,kwa ujasiri!22Ndipo kwato za farasi zikafanya mshindo:farasi wake wenye nguvuhuenda mbio kwa kurukaruka.23Malaika wa Mwenyezi Mungu akasema, ‘Laani Merozi.Laani watu wake kwa uchungu,kwa kuwa hawakuja kumsaidia Mwenyezi Mungu,kumsaidia Mwenyezi Mungu dhidi ya hao wenye nguvu.’24“Yaeli abarikiwe kuliko wanawake wote,mkewe Heberi, Mkeni,abarikiwe kuliko wanawake wotewanaoishi kwenye mahema.25Sisera alimwomba maji, naye akampa maziwa;kwenye bakuli la heshimaakamletea maziwa mgando.26Akanyoosha mkono wakeakashika kigingi cha hema,mkono wake wa kuumeukashika nyundo ya fundi.Akampiga Sisera kwa nyundo,akamponda kichwa chake,akamvunjavunja na kumtoboapaji lake la uso.27Aliinama miguuni pa Yaeli,akaanguka; akalala hapo.Alipoinama miguuni pake,alianguka;pale alipoinamia, ndipo alipoanguka,akiwa amekufa.28“Kupitia dirishani mamaye Sisera alichungulia;nyuma ya dirisha alilia, akasema,‘Mbona gari lake la vita linachelewa kufika?Mbona vishindo vya magari yake ya vitavimechelewa?’29Wajakazi wale wenye busarakuliko wengine wote wanamjibu;naam, naye anasema moyoni mwake,30‘Je, hawapati na kugawanya nyara:msichana mmoja au wawili kwa kila mtu,mavazi ya rangi mbalimbali kwa Sisera kuwa nyara,mavazi ya rangi mbalimbali yaliyotariziwa,mavazi yaliyotariziwa vizuri kwa ajili ya shingo yangu:haya yote yakiwa nyara?’31“Adui zako wote na waangamie hivyo, Ee Mwenyezi Mungu!Bali wote wanaokupenda na wawe kama jualinavyochomoza kwa nguvu zake.”Hivyo nchi ikawa na amani kwa miaka arobaini.