Yoshua13swh_onmm
Sehemu za Kanaani ambazo hazijatwaliwa
1Yoshua alipokuwa mzee, umri wake ukiwa umesogea sana, Mwenyezi Mungu akamwambia, “Wewe ni mzee sana, na bado imesalia sehemu kubwa sana ya nchi ambayo haijatwaliwa.2“Nchi iliyosalia ni hii:“maeneo yote ya Wafilisti na Wageshuri:3kutoka Mto Shihori ulioko mashariki mwa Misri, kuelekea kaskazini kwenye eneo la Ekroni, ambayo yote ilihesabika kama ya Wakanaani, maeneo yale matano ya watawala wa Wafilisti, ambayo ni Gaza, Ashdodi, Ashkeloni, Gathi na Ekroni; nchi ya Waavi4kuanzia kusini; nchi yote ya Wakanaani, kuanzia Ara ambayo ni ya Wasidoni, ikienea hadi Afeki, na eneo la Waamori,5eneo la Wagebali; na Lebanoni yote kuelekea mashariki, kuanzia Baal-Gadi chini ya Mlima Hermoni hadi Lebo-Hamathi.6“Na kuhusu wakaaji wote katika maeneo ya milima, kuanzia Lebanoni hadi Misrefoth-Maimu, pamoja na eneo lote la Wasidoni, mimi mwenyewe nitawafukuza, niwaondoe kwa ajili ya Waisraeli. Hakikisha umegawa nchi hii kwa Israeli kuwa urithi, kama nilivyokuagiza,7sasa basi, ligawanye eneo hili kwa yale makabila tisa na ile nusu ya kabila la Manase kuwa urithi.”