Yohana5
Isa amponya mtu kwenye Bwawa la Bethzatha
1Baada ya haya, kulikuwa na Sikukuu ya Wayahudi, naye Isa akapanda kwenda Yerusalemu.2Huko Yerusalemu, karibu na mlango uitwao Mlango wa Kondoo, palikuwa na bwawa moja lililoitwa Bethzatha kwa Kiebrania, ambalo lilikuwa limezungukwa na makumbi matano.3Hapa palikuwa na idadi kubwa ya wasiojiweza, yaani vipofu, viwete, na waliopooza [wakingojea maji yatibuliwe.4Kwa maana malaika alikuwa akishuka wakati fulani, akayatibua maji. Yule angekuwa wa kwanza kuingia ndani baada ya maji kutibuliwa alipona ugonjwa wowote aliokuwa nao] .5Mtu mmoja aliyekuwa ameugua kwa miaka thelathini na nane alikuwa hapo.6Isa alipomwona akiwa amelala hapo, na akijua amekuwa katika hali hiyo kwa muda mrefu, akamwambia, “Je, wataka kuponywa?”7Yule mgonjwa akamjibu, “Bwana , mimi sina mtu wa kuniingiza bwawani maji yanapotibuliwa. Nami ninapotaka kutumbukia bwawani, mtu mwingine huingia kabla yangu.”8Isa akamwambia, “Inuka! Chukua mkeka wako na uende.”9Mara yule mtu akapona, akachukua mkeka wake, akaanza kutembea.Basi siku hiyo ilikuwa siku ya Sabato.10Kwa hiyo viongozi wa Wayahudi wakamwambia yule mtu aliyeponywa, “Leo ni Sabato; si halali wewe kubeba mkeka wako.”11Yeye akawajibu, “Yule mtu aliyeniponya aliniambia, ‘Chukua mkeka wako na uende.’ ”12Wakamuuliza, “Ni mtu gani huyo aliyekuambia uchukue mkeka wako uende?”13Basi yule mtu aliyeponywa hakufahamu ni nani aliyemponya, kwa sababu Isa alikuwa amepotea ndani ya umati ule wa watu waliokuwa hapo.14Baadaye Isa akamkuta yule mtu aliyemponya ndani ya Hekalu na kumwambia, “Tazama umeponywa. Usitende dhambi tena, lisije likakupata jambo baya zaidi.”15Yule mtu akaenda, akawaambia wale viongozi wa Wayahudi kuwa ni Isa aliyemponya.