Ayubu39swh_onmm

Mwenyezi Mungu anaendelea kumjibu Ayubu

1“Je, unajua wakati mbuzi wa mlimani wanapozaa?Je, unatambua wakati kulungu jike anapozaa mtoto wake?2Je, unaweza kuhesabu miezi hadi wanapozaa?Je, unajua majira yao ya kuzaa?3Wao hujiinamisha na kuzaa watoto wao;uchungu wa kuzaa unakoma.4Watoto wao hustawi na kuongezeka nguvu nyikani;huenda zao wala hawarudi tena.
5“Ni nani aliyemwachia punda-mwitu awe huru?Ni nani aliyezifungua kamba zake?6Nimempa nchi isiyokaliwa na watu kuwa masikani yake,nchi ya chumvi kuwa makao yake.7Huzicheka ghasia za mji,wala hasikii kelele za mwendesha gari.8Huzunguka vilimani kwa ajili ya malishona kutafuta kila kitu kibichi.
9“Je, nyati atakubali kukutumikia?Atakaa karibu na hori lako usiku?10Je, unaweza kumfungia kwenye matuta kwa kamba?Je, atalima mabonde nyuma yako?11Je, utamtumainia kwa ajili ya nguvu zake nyingi?Utamwachia yeye kazi zako nzito?12Utaweza kumwamini akuletee nafaka yako nyumbanikutoka shambani na kuikusanya kwenye sakafu yako ya kupuria?
13“Mbuni hupigapiga mabawa yake kwa furaha,lakini hayawezi kulinganishwana mabawa na manyoya ya korongo.14Huyataga mayai yake juu ya ardhi,na kuyaacha yapate joto mchangani,15bila kujali kuwa mguu unaweza kuyaponda,kwamba baadhi ya wanyama wa porini wanaweza kuyakanyaga.16Yeye huyafanyia makinda yake ukatili kama vile si yake;hajali kwamba taabu yake inaweza ikawa bure,17kwa kuwa Mungu hakumjalia hekima,wala hakumpa fungu la akili njema.18Lakini akunjuapo mabawa yake kukimbia,humcheka farasi pamoja na yeye aliyempanda.
19“Je, wewe humpa farasi nguvuau kuivika shingo yake manyoya marefu?20Je, wewe humfanya farasi aruke kama nzige,akistaajabisha kwa tishio la mlio wake wa majivuno?21Huparapara bila woga, akizifurahia nguvu zake,husonga mbele kukabiliana na silaha.22Huicheka hofu, haogopi chochote,wala haukimbii upanga.23Podo hutoa sauti kando yake,pamoja na mkuki unaong’aa na fumo.24Bila woga na kwa ghadhabu huimeza nchi,wala tarumbeta iliapo yeye hawezi kusimama.25Asikiapo sauti ya baragumu yeye hulia, ‘Aha!’Hunusa harufu ya vita toka mbali,husikia sauti ya mtoa amri na kelele za vita.
26“Je, mwewe huruka kwa hekima yakona kuyakunjua mabawa yake kuelekea kusini?27Je, tai hupaa juu kwa amri yakona kujenga kiota chake mahali pa juu?28Huishi juu ya miamba mirefu na kukaa huko usiku;majabali yenye ncha kali ndiyo ngome yake.29Kutoka huko hutafuta chakula chake;macho yake hukiona kutoka mbali.30Makinda yake hujilisha damu,na pale palipo na machinjo, ndipo yeye alipo.”