Yeremia49swh_onmm

Ujumbe kuhusu Amoni

1Kuhusu Waamoni:
Hili ndilo asemalo Mwenyezi Mungu:
“Je, Israeli hana wana?Je, hana warithi?Kwa nini basi Moleki amechukua milki ya Gadi?Kwa nini watu wake wanaishi katika miji yake?
2Lakini siku zinakuja,”asema Mwenyezi Mungu,“nitakapopiga ukelele wa vitadhidi ya Raba, mji wa Waamoni;utakuwa kilima cha magofu,navyo vijiji vinavyouzungukavitateketezwa kwa moto.Kisha Israeli atawafukuzawale waliomfukuza,”asema Mwenyezi Mungu.3“Lia kwa huzuni, ee Heshboni, kwa kuwa Ai umeangamizwa!Pigeni kelele, enyi wakazi wa Raba!Vaeni gunia na kuomboleza,kimbieni hapa na pale ndani ya kuta,kwa kuwa Moleki ataenda uhamishoni,yeye pamoja na makuhani na maafisa wake.4Kwa nini unajivunia mabonde yako,kujivunia mabonde yako yaliyozaa sana?Ee binti usiye mwaminifu,unayeutumainia utajiri wako na kusema,‘Ni nani atakayenishambulia?’5Nitaleta hofu kuu juu yakokutoka kwa wale wote wanaokuzunguka,”asema Mwenyezi Mungu, Mungu wa majeshi ya mbinguni.“Kila mmoja wenu ataondolewa,wala hakuna hata mmoja atakayekusanya wakimbizi.
6“Lakini hatimaye,nitarudisha mateka wa Waamoni,”asema Mwenyezi Mungu.

Ujumbe kuhusu Edomu

7Kuhusu Edomu:
Hili ndilo asemalo Mwenyezi Mungu, Mungu wa majeshi ya mbinguni:
“Je, hakuna tena hekima katika Temani?Je, shauri limewapotea wenye busara?Je, hekima yao imechakaa?
8Geuka na ukimbie, jifiche katika mapango marefu kabisa,wewe uishiye Dedani,kwa kuwa nitaleta maafa juu ya Esauwakati nitakapomwadhibu.9Je, kama wachuma zabibu wangekuja kwako,wasingebakiza zabibu chache?Kama wezi wangekujia usiku,je, si wangeiba tu kiasi ambacho wangehitaji?10Lakini nitamvua Esau nguo abaki uchi,nitayafunua maficho yake,ili asiweze kujificha.Watoto wake, jamaa na majirani wataangamia,naye hatakuwepo tena.11Waache yatima wako; nitayalinda maisha yao.Wajane wako piawanaweza kunitumaini mimi.”12Hili ndilo asemalo Mwenyezi Mungu: “Kama wasiostahili kukinywea kikombe ni lazima wakinywe, kwa nini wewe usiadhibiwe? Hutakwepa kuadhibiwa, ni lazima ukinywe.13Ninaapa kwa nafsi yangu,” asema Mwenyezi Mungu, “kwamba Bosra utakuwa magofu na kitu cha kutisha, cha aibu na cha kulaania; miji yake yote itakuwa magofu milele.”14Nimesikia ujumbe kutoka kwa Mwenyezi Mungu:Mjumbe alitumwa kwa mataifa kusema,“Jikusanyeni ili kuushambulia!Inukeni kwa ajili ya vita!”
15“Sasa nitakufanya mdogo miongoni mwa mataifa,uliyedharauliwa miongoni mwa watu.16Vitisho vyako na kiburi cha moyo wakovimekudanganya,wewe unayeishi katika majabali ya miamba,wewe unayedumu katika miinuko ya kilima.Ujapojenga kiota chako juu sana kama cha tai,nitakushusha chini kutoka huko,”asema Mwenyezi Mungu.17“Edomu atakuwa kitu cha kutisha;wote wapitao karibuwatashangaa na kuzomeakwa sababu ya majeraha yake yote.18Kama vile Sodoma na Gomora zilivyoangamizwa,pamoja na miji iliyokuwa jirani nayo,”asema Mwenyezi Mungu,“vivyo hivyo hakuna mtu yeyote atakayeishi humo.Naam, hakuna mtu yeyote atakayekaa humo.
19“Kama simba anayepanda kutoka vichaka vya Yordanikuja kwenye nchi ya malisho mengi,ndivyo nitakavyomfukuza Edomu kutoka nchi yake ghafula.Ni nani aliye mteule nitakayemweka kwa ajili ya jambo hili?Ni nani aliye kama mimi,na ni nani awezaye kunipinga?Tena ni mchungaji yupi awezayekusimama kinyume nami?”20Kwa hiyo, sikia kile Mwenyezi Mungu alichokipanga dhidi ya Edomu,kile alichokusudia dhidi ya wale wanaoishi Temani:Aliye mchanga katika kundi ataburutwa mbali;yeye ataharibu kabisa malisho yao kwa sababu yao.21Kwa sauti ya anguko lao, dunia itatetemeka.Kilio chao kitasikika hadi Bahari ya Shamu .22Tazama! Tai atapaa juu angani na kuruka chini kwa ghafula,akitandaza mabawa yake juu ya Bosra.Katika siku hiyo, mioyo ya mashujaa wa Edomuitakuwa kama moyo wa mwanamke katika uchungu wa kuzaa.

Ujumbe kuhusu Dameski

23Kuhusu Dameski:“Hamathi na Arpadi imetahayarika,kwa kuwa wamesikia habari mbaya.Wamevunjika moyo na wametaabikakama bahari iliyochafuka.24Dameski amedhoofika,amegeuka na kukimbia,hofu ya ghafula imemkamata sana;amepatwa na uchungu na maumivu,maumivu kama ya mwanamke katika uchungu wa kuzaa.25Kwa nini mji unaosifika haujaachwa,mji wenye sifa, na wa furaha yangu?26Hakika, vijana wake wanaume wataanguka barabarani;askari wake wote watanyamazishwa siku hiyo,”asema Mwenyezi Mungu, Mungu wa majeshi ya mbinguni.27“Nitatia moto kuta za Dameski;utaangamiza ngome za Ben-Hadadi.”

Ujumbe kuhusu Kedari na Hazori

28Kuhusu Kedari na falme za Hazori, ambazo Nebukadneza mfalme wa Babeli alizishambulia:
Hili ndilo asemalo Mwenyezi Mungu:
“Inuka, ushambulie Kedarina kuwaangamiza watu wa mashariki.
29Mahema yao na makundi yao ya kondoo yatachukuliwa;vibanda vyao vitatwaliwa,pamoja na mali yao yote na ngamia wao.Watu watawapigia kelele,‘Hofu kuu iko kila upande!’
30“Kimbieni haraka!Kaeni kwenye mapango marefu sana, ninyi mnaoishi Hazori,”asema Mwenyezi Mungu.“Nebukadneza, mfalme wa Babeli amepanga njama dhidi yenu;amebuni hila dhidi yenu.
31“Inuka na ulishambulie taifa lililostarehe,linaloishi kwa kujiamini,”asema Mwenyezi Mungu,“taifa lisilo na malango wala makomeo;watu wake wanaishi peke yao.32Ngamia wao watakuwa nyara,nayo mifugo yao itatekwa.Walio maeneo ya mbalinitawatawanya pande zote,nami nitaleta maafa juu yaokutoka kila upande,”asema Mwenyezi Mungu.33“Hazori itakuwa makao ya mbweha,mahali pa ukiwa milele.Hakuna atakayeishi humo;hakuna mtu atakayekaa ndani yake.”

Ujumbe kuhusu Elamu

34Hili ndilo neno la Mwenyezi Mungu lililomjia nabii Yeremia kuhusu Elamu, mapema katika utawala wa Sedekia mfalme wa Yuda:
35Hili ndilo asemalo Mwenyezi Mungu, Mungu wa majeshi ya mbinguni:“Tazama, nitavunja upinde wa Elamu,ulio tegemeo la nguvu zao.36Nitaleta pepo nne dhidi ya Elamutoka pande nne za mbingu,nitawatawanya katika hizo pande nne,wala hapatakuwa na taifaambalo watu wa Elamu waliofukuzwahawataenda.37Nitamfadhaisha Elamu mbele ya adui zao,mbele yao wanaoutafuta uhai wao;nitaleta maafa juu yao,naam, hasira yangu kali,”asema Mwenyezi Mungu.“Nitawafuatia kwa upangahadi nitakapowamaliza.38Nitaweka kiti changu cha enzi huko Elamuna kumwangamiza mfalme wake na maafisa wake,”asema Mwenyezi Mungu.
39“Lakini nitarudisha mateka wa Elamukatika siku zijazo,”asema Mwenyezi Mungu.