Yeremia4swh_onmm
1“Ikiwa utataka kurudi, ee Israeli,nirudie mimi,”asema Mwenyezi Mungu.“Ikiwa utaondoa sanamu zako za kuchukiza mbele ya macho yanguna usiendelee kutangatanga,2ikiwa utaapa katika kweli, kwa haki na kwa unyofu,‘Hakika kama Mwenyezi Mungu aishivyo,’ndipo mataifa yatakapobarikiwa naye,na ndani yake watajitukuza.”3Hili ndilo asemalo Mwenyezi Mungu kwa watu wa Yuda na kwa Yerusalemu:“Vunjeni mabonge kwenye mashamba yenu,wala msipande katikati ya miiba.4Jitahirini katika Mwenyezi Mungu,tahirini mioyo yenu,enyi wanaume wa Yudana watu wa Yerusalemu,la sivyo ghadhabu yangu itatoka kwa nguvuna kuwaka kama motokwa sababu ya uovu mliotenda,ikiwaka pasipo wa kuizima.