Yeremia2swh_onmm

Israeli amwacha Mwenyezi Mungu

1Neno la Mwenyezi Mungu lilinijia kusema,2“Nenda ukahubiri masikioni mwa watu wa Yerusalemu:
“Hivi ndivyo asemavyo Mwenyezi Mungu:
“ ‘Nakumbuka moyo wako wa uchaji katika ujana wako,jinsi ulivyonipenda kama bibi arusina kunifuata katika jangwa lile lote,katika nchi isiyopandwa mbegu.
3Israeli alikuwa mtakatifu kwa Mwenyezi Mungu,kama malimbuko ya kwanza ya mavuno yake;wote waliomwangamiza walihesabiwa kuwa na hatia,nayo maafa yaliwakumba,’ ”asema Mwenyezi Mungu.
4Sikia neno la Mwenyezi Mungu, ee nyumba ya Yakobo,nanyi nyote jamaa za nyumba ya Israeli.5Hivi ndivyo asemavyo Mwenyezi Mungu:“Je, baba zenu waliona kosa gani kwangu,hata wakatangatanga mbali nami hivyo?Walifuata sanamu batili,nao wenyewe wakawa batili.6Hawakuuliza, ‘Yuko wapi Mwenyezi Mungu,aliyetupandisha kutoka Misrina kutuongoza kupitia nyika kame,kupitia nchi ya majangwa na mabonde,nchi ya ukame na giza,nchi ambayo hakuna mtu asafiriye ndani yakewala hakuna mtu aishiye humo?’7Niliwaleta katika nchi yenye wingi wa vituili mpate kula matunda yakena utajiri wa mazao yake.Lakini mkaja na kuinajisi nchi yangu,na kuufanya urithi wangu chukizo.8Makuhani hawakuuliza,‘Yuko wapi Mwenyezi Mungu?’Wale wanaoshughulikia sheria hawakunijua mimi;viongozi waliasi dhidi yangu.Manabii walitabiri kwa jina la Baali,wakifuata sanamu batili.
9“Kwa hiyo naleta tena mashtaka dhidi yako,”asema Mwenyezi Mungu.“Nami nitaleta mashtaka dhidi ya watoto wa watoto wako.10Vuka, nenda ng’ambo hadi pwani ya Kitimu nawe uangalie,tuma watu waende Kedari, wachunguze kwa makini,uone kama kumeshawahi kuwa kitu kama hiki.11Je, taifa limebadili miungu yake wakati wowote?(Hata ingawa hao si miungu kamwe.)Lakini watu wangu wamebadili Utukufu waokwa sanamu batili.12Shangaeni katika hili, ee mbingu,nanyi tetemekeni kwa hofu kuu,”asema Mwenyezi Mungu.13“Watu wangu wametenda dhambi mbili:Wameniacha mimi,niliye chemchemi ya maji yaliyo hai,nao wamejichimbia visima vyao wenyewe,visima vilivyobomoka, visivyoweza kuhifadhi maji.14Je, Israeli ni mtumishi, yaani mtumwa kwa kuzaliwa?Kwa nini basi amekuwa mateka?15Simba wamenguruma;wamemngurumia.Wameifanya nchi yake kuwa ukiwa;miji yake imeteketezwa, nayo imeachwa haina watu.16Pia watu wa Memfisi na Tapanesiwamekupiga fuvu la kichwa.17Je, hukujiletea hili wewe mwenyewekwa kumwacha Mwenyezi Mungu, Mungu wakoalipowaongoza njiani?18Sasa kwa nini uende Misrikunywa maji ya Shihori ?Nawe kwa nini kwenda Ashurukunywa maji ya Mto ?19Uovu wako utakuadhibu;kurudi nyuma kwako kutakukemea.Basi kumbuka, utambuejinsi lilivyo jambo ovu na chungu kwakounapomwacha Mwenyezi Mungu, Mungu wako,na kutokuwa na hofu yangu,”asema Mwenyezi Mungu, Mungu wa majeshi ya mbinguni.
20“Zamani nilivunja nira yakona kukatilia mbali vifungo vyako;ukasema, ‘Sitakutumikia!’Hakika, kwenye kila kilima kirefuna chini ya kila mti uliotanda matawi yakeulijilaza kama kahaba.21Nilikupanda ukiwa mzabibu ulio bora sana,mkamilifu na wa mbegu nzuri.Ilikuwaje basi ukawa kinyume nami,ukaharibika na kuwa mzabibu mwitu?22Hata ujisafishe kwa magadina kutumia sabuni nyingi,bado doa la hatia yako liko mbele zangu,”asema Bwana Mungu Mwenyezi.23“Wawezaje kusema, ‘Mimi si najisi,sijawafuata Mabaali’?Kumbuka jinsi ulivyotenda kule bondeni;fikiri uliyoyafanya.Wewe ni ngamia jike mwenye mbioukikimbia hapa na pale,24punda-mwitu aliyezoea jangwa,anayenusa upepo katika tamaa yake kubwa:wakati wake wa kuhitaji mbeguni nani awezaye kumzuia?Madume yoyote yanayomfuatiliahayana haja ya kujichosha;wakati wa kupandwa kwake yatampata tu.25Usikimbie hadi miguu yako iwe haina viatu,na koo lako liwe limekauka.Lakini ulisema, ‘Haina maana!Ninaipenda miungu ya kigeni,nami lazima niifuatie.’
26“Kama vile mwizi anavyoaibika akikamatwa,hivyo ndivyo nyumba ya Israeli inavyoaibishwa:wao wenyewe, wafalme wao na maafisa wao,makuhani wao na manabii wao.27Wanaiambia miti, ‘Wewe ndiwe baba yangu,’nalo jiwe, ‘Wewe ndiwe uliyenizaa.’Wamenipa visogo vyaowala hawakunigeuzia nyuso zao;lakini wakiwa katika taabu, wanasema,‘Njoo utuokoe!’28Iko wapi basi ile miungu mliyojitengenezea?Yenyewe na ije kama inaweza kuwaokoawakati mko katika taabu!Kwa maana mna miungu mingikama mlivyo na miji, ee Yuda.
29“Kwa nini mnaleta mashtaka dhidi yangu?Ninyi nyote mmeniasi,”asema Mwenyezi Mungu.30“Nimeadhibu watu wako bure tu,hawakujirekebisha.Upanga wako umewala manabii wakokama simba mwenye njaa.31“Enyi wa kizazi hiki, tafakarini neno la Mwenyezi Mungu:“Je, nimekuwa jangwa kwa Israeliau nchi ya giza nene?Kwa nini watu wangu wanasema, ‘Sisi tuko huru kuzurura,hatutarudi kwako tena’?32Je, mwanamwali husahau vito vyake,au bibi arusi mapambo yake ya arusi?Lakini watu wangu wamenisahau mimi,tena kwa siku zisizo na hesabu.33Je, wewe una ustadi kiasi gani katika kufuatia mapenzi!Hata wale wanawake wabaya kuliko wotewanaweza kujifunza kutokana na njia zako.34Katika nguo zako watu huonadamu ya uhai ya maskini wasio na hatia,ingawa hukuwakamata wakivunja nyumba.Lakini katika haya yote35unasema, ‘Sina hatia;Mungu hajanikasirikia.’Lakini nitakuhukumu kwa sababu unasema,‘Mimi sijatenda dhambi.’36Kwa nini unatangatanga sana,ukibadili njia zako?Utakatishwa tamaa na Misrikama ulivyokatishwa na Ashuru.37Pia utaondoka mahali hapoukiwa umeweka mikono kichwani,kwa kuwa Mwenyezi Mungu amewakataa wale unaowatumainia;hutasaidiwa nao.