Yeremia15

Adhabu isiyoepukika

1Kisha Mwenyezi Mungu akaniambia: “Hata kama Musa na Samweli wangesimama mbele zangu, moyo wangu usingewaelekea watu hawa. Waondoe mbele za macho yangu! Waache waende!2Nao wakikuuliza, ‘Twende wapi?’ Waambie, ‘Hili ndilo asemalo Mwenyezi Mungu:“ ‘Wale waliowekwa kwa ajili ya kufa, na wafe;waliowekewa kufa kwa upanga, kwa upanga;waliowekewa kufa kwa njaa, kwa njaa;na waliowekewa kupelekwa uhamishoni,wapelekwe uhamishoni.’ ”
3Mwenyezi Mungu asema, “Nitatuma aina nne za waangamizi: upanga ili kuua, mbwa ili kukokota mbali, ndege wa angani na wanyama wa nchi ili wale na waangamize.4Nitawafanya wawe machukizo kwa falme zote za dunia kwa sababu ya kile alichofanya Manase mwana wa Hezekia mfalme wa Yuda huko Yerusalemu.5“Ni nani atakayekuhurumia, ee Yerusalemu?Ni nani atakayeomboleza kwa ajili yako?Ni nani atakayesimama ili kuulizakuhusu hali yako?6Umenikataa mimi,” asema Mwenyezi Mungu.“Unazidi kukengeuka.Hivyo nitanyoosha mkono wangu juu yako na kukuangamiza,siwezi kuendelea kukuonea huruma.7Nitawapepeta kwa ungokwenye malango ya miji ya nchi.Nitaleta msiba na maangamizi juu ya watu wangu,kwa maana hawajabadili njia zao.8Nitawafanya wajane wao kuwa wengikuliko mchanga wa bahari.Wakati wa adhuhuri nitamleta mwangamizidhidi ya mama wa vijana wao wa kiume;kwa ghafula nitaleta juu yaomaumivu makuu na hofu kuu.9Mama mwenye watoto saba atazimiana kupumua pumzi yake ya mwisho.Jua lake litatua kukiwa bado mchana,atatahayarika na kufedheheka.Wale wote waliobaki nitawaua kwa upangambele ya adui zao,”asema Mwenyezi Mungu.
10Ole wangu, mama yangu, kwamba ulinizaa,mtu ambaye ulimwengu woteunashindana na kugombana naye!Sikukopa wala sikukopesha,lakini kila mmoja ananilaani.
11Mwenyezi Mungu akasema,“Hakika nitakuokoa kwa kusudi jema,hakika nitawafanya adui zako wakuombe msaadanyakati za maafa na nyakati za dhiki.
12“Je, mtu aweza kuvunja chuma,chuma kinachotoka kaskazini, au avunje shaba?
13“Utajiri wako na hazina zako nitavitoa kuwa nyara,bila gharama,kwa sababu ya dhambi zako zotekatika nchi yako yote.14Nitakufanya uwe mtumwa wa adui zakokatika nchi usiyoijua,kwa kuwa katika hasira yangu moto umewashwautakaowaka juu yako daima.”
15Wewe unafahamu, Ee Mwenyezi Mungu,unikumbuke na unitunze mimi.Lipiza kisasi juu ya watesi wangu.Kwa uvumilivu wako usiniondolee mbali;kumbuka jinsi ninavyoshutumiwa.16Maneno yako yalipokuja, niliyala;yakawa shangwe yanguna furaha ya moyo wangu,kwa kuwa nimeitwa kwa jina lako,Ee Bwana Mwenyezi Mungu,Mungu wa majeshi ya mbinguni.17Kamwe sikuketi katika kundi la wafanyao sherehe,wala kamwe sikujifurahisha pamoja nao;niliketi peke yangu kwa sababu mkono wako ulikuwa juu yangu,na wewe ulikuwa umenijaza hasira.18Kwa nini maumivu yangu hayakomi,na jeraha langu ni la kuhuzunisha,wala haliponyeki?Je, utakuwa kwangu kama kijito cha udanganyifu,kama chemchemi iliyokauka?
19Kwa hiyo hili ndilo asemalo Mwenyezi Mungu:“Ukitubu, nitakurejeshaili uweze kunitumikia;ukinena maneno yenye maana,wala si ya upuzi,utakuwa mnenaji wangu.Watu hawa ndio watakaokugeukia,wala si wewe utakayewageukia wao.20Nitakufanya wewe uwe ukuta kwa watu hawa,ngome ya ukuta wa shaba;watapigana nawelakini hawatakushinda,kwa maana mimi niko pamoja nawekukuponya na kukuokoa,”asema Mwenyezi Mungu.21“Nitakuokoa kutoka mikono ya waovu,na kukukomboa kutoka makucha ya watu wakatili.”