Yeremia13swh_onmm

Mkanda wa kitani

1Hili ndilo Mwenyezi Mungu aliloniambia: “Nenda ununue mkanda wa kitani, ujivike kiunoni mwako, lakini usiuache uguse maji.”2Kwa hiyo nikanunua mkanda, kama Mwenyezi Mungu alivyoniagiza, nikajivika kiunoni.3Ndipo neno la Mwenyezi Mungu likanijia kwa mara ya pili:4“Chukua mkanda ulionunua ambao umeuvaa kiunoni mwako, uende sasa Frati uufiche ndani ya ufa mdogo kwenye mwamba.”5Ndipo nikaenda na kuuficha ule mkanda huko Frati, kama Mwenyezi Mungu alivyoniamuru.6Baada ya siku nyingi Mwenyezi Mungu akaniambia, “Nenda sasa Frati ukauchukue ule mkanda niliokuambia uufiche huko.”7Hivyo nikaenda Frati na kuuchimbua ule mkanda kutoka pale nilipokuwa nimeuficha, lakini sasa ulikuwa umeharibika na haufai tena kabisa.8Ndipo neno la Mwenyezi Mungu likanijia:9“Hili ndilo asemalo Mwenyezi Mungu: ‘Vivyo hivyo ndivyo nitakavyokiharibu kiburi cha Yuda na kiburi kikuu cha Yerusalemu.10Watu hawa waovu, wanaokataa kusikiliza maneno yangu, wafuatao ukaidi wa mioyo yao na kufuata miungu mingine wakiitumikia na kuiabudu, watakuwa kama mshipi huu ambao haufai kabisa!11Kwa maana kama vile mshipi ufungwavyo kiunoni mwa mtu, ndivyo nilivyoifunga nyumba yote ya Israeli na nyumba yote ya Yuda,’ asema Mwenyezi Mungu, ‘ili wawe watu wangu kwa ajili ya utukufu wangu, sifa na heshima yangu. Lakini hawajasikiliza.’

Viriba vya mvinyo

12“Waambie: ‘Hili ndilo Mwenyezi Mungu, Mungu wa Israeli, asemalo: kila kiriba inapasa kijazwe mvinyo.’ Wakikuambia, ‘Kwani hatujui kwamba kila kiriba inapasa kijazwe mvinyo?’13Uwaambie, ‘Hili ndilo asemalo Mwenyezi Mungu: nitawajaza ulevi wote wanaoishi katika nchi hii, pamoja na wafalme wanaoketi kwenye kiti cha ufalme cha Daudi, makuhani, manabii na wakaaji wote wa Yerusalemu.14Nitawagombanisha kila mmoja na mwenzake, baba na wana wao, asema Mwenyezi Mungu. Sitawarehemu wala kuwahurumia ili niache kuwaangamiza.’ ”

Tishio la kutekwa

15Sikieni na mzingatie,msiwe na kiburi,kwa kuwa Mwenyezi Mungu amenena.16Mpeni utukufu Mwenyezi Mungu, Mungu wenu,kabla hajaleta giza,kabla miguu yenu haijajikwaajuu ya vilima vitakavyotiwa giza.Mlitarajia nuru,lakini ataifanya kuwa giza nenena kuibadili kuwa huzuni kubwa.17Lakini kama hamtasikiliza,nitalia sirinikwa ajili ya kiburi chenu;macho yangu yatalia kwa uchungu,yakitiririka machozi,kwa sababu kundi la kondoo la Mwenyezi Mungulitachukuliwa mateka.
18Mwambie mfalme na mama malkia,“Shukeni kutoka viti vyenu vya utawala,kwa kuwa taji zenu za utukufuzitaanguka kutoka vichwani mwenu.”19Miji ya Negebu itafungwa,wala hapatakuwa na mtu wa kuifungua.Watu wa Yuda wote watapelekwa uhamishoni,wakichukuliwa kabisa waende mbali.
20Inua macho yako uonewale wanaokuja kutoka kaskazini.Liko wapi lile kundi ulilokabidhiwa,wale kondoo uliojivunia?21Utasema nini Mwenyezi Mungu atakapowaweka juu yakowale ulioungana nao kama rafiki zako maalum?Je, hutapatwa na uchungu kama mwanamkealiye katika uchungu wa kuzaa?22Nawe ukijiuliza,“Kwa nini haya yamenitokea?”Ni kwa sababu ya dhambi zako nyingimarinda yako yameraruliwana mwili wako umetendewa vibaya.23Je, Mkushi aweza kubadili ngozi yakeau chui kubadili madoadoa yake?Vivyo hivyo, wewe uliyezoea kutenda mabayahuwezi kufanya mema.
24“Nitawatawanya kama makapiyapeperushwayo na upepo wa jangwani.25Hii ndiyo kura yako,fungu nililokuamulia,”asema Mwenyezi Mungu,“kwa sababu umenisahau mimina kuamini miungu ya uongo.26Nitayafunua marinda yako juu ya uso wakoili aibu yako ionekane,27yaani uzinzi wako na kulia kwako kulikojaa tamaa kama farasi,na ukahaba wako usio na aibu!Nimeyaona matendo yako ya machukizojuu ya vilima na mashambani.Ole wako, ee Yerusalemu!Utaendelea kuwa najisi hadi lini?”