1Sikieni lile Mwenyezi Mungu anasema nanyi, ee nyumba ya Israeli.2Hili ndilo asemalo Mwenyezi Mungu:“Usijifunze njia za mataifawala usitishwe na ishara katika anga,ingawa mataifa yanatishwa nazo.3Kwa maana desturi za mataifa hazina maana,wanakata mti msituni,na fundi anauchonga kwa patasi.4Wanauremba kwa fedha na dhahabu,wanaukaza kwa nyundo na misumari ili usitikisike.5Sanamu zao ni kama kinyagokilichowekwa katika shamba la matango kutishia ndege,nazo haziwezi kuongea;na kwa kuwa haziwezi kutembea zinabebwa.Usiziogope. Haziwezi kudhuruwala kutenda lolote jema.”6Hakuna aliye kama wewe, Ee Mwenyezi Mungu;wewe ni mkuu,jina lako ni lenye nguvu na uweza.7Ni nani ambaye haimpasi kukuheshimu wewe,Ee Mfalme wa mataifa?Hii ni stahili yako.Miongoni mwa watu wote wenye hekimakatika mataifa na katika falme zao zote,hakuna aliye kama wewe.8Wote hawana akili, tena ni wapumbavu;wanafundishwa na sanamu batili za miti.9Huleta fedha iliyofuliwa kutoka Tarshishina dhahabu kutoka Ufazi.Kile ambacho fundi na sonara wametengenezahuvikwa mavazi ya rangi ya samawi na urujuani:vyote vikiwa vimetengenezwana mafundi stadi.10Lakini Mwenyezi Mungu ni Mungu wa kweli,yeye ndiye Mungu aliye hai, Mfalme wa milele.Anapokasirika, dunia hutetemeka,mataifa hayawezi kustahimili hasira yake.11“Waambie hivi: ‘Miungu hii, ambayo haikuumba mbingu na dunia, itaangamia duniani na chini ya mbingu.’ ”12Lakini Mungu aliiumba dunia kwa uweza wake,akaweka misingi ya ulimwengu kwa hekima yake,na akazitandaza mbingu kwa ufahamu wake.13Atoapo sauti yake, maji yaliyo katika mbingu hunguruma;huyafanya mawingu yainuke kutoka miisho ya dunia.Hupeleka miali ya radi pamoja na mvua,naye huuleta upepo kutoka ghala zake.14Kila mtu ni mjinga na hana maarifa;kila sonara ameaibishwa na sanamu zake.Vinyago vyake ni vya udanganyifu;havina pumzi.15Ni ubatili tu, vitu vya kufanyia mzaha;wakati wa hukumu yao, wataangamia.16Yeye aliye Fungu la Yakobo sivyo alivyo,kwani ndiye Muumba wa vitu vyote,pamoja na Israeli, kabila la urithi wake:Mwenyezi Mungu, Mungu wa majeshi ya mbinguni ndilo jina lake.
Maangamizi yajayo
17Kusanyeni mali na vitu vyenu mwondoke nchi hii,enyi mnaoishi katika hali ya kuzingirwa na jeshi.18Kwa kuwa hili ndilo asemalo Mwenyezi Mungu:“Wakati huu, nitawatupa nje kwa nguvuwote wanaoishi katika nchi hii;nitawataabishaili wapate kutekwa.”19Ole wangu mimi kwa ajili ya kuumia kwangu!Jeraha langu ni kubwa!Lakini nilisema,“Kweli hii ni adhabu yangu,nami sharti niistahimili.”20Hema langu limeangamizwa;kamba zake zote zimekatwa.Wana wangu wametekwa na hawapo tena;hakuna hata mmoja aliyebaki wa kusimamisha hema languwala wa kusimamisha kibanda changu.21Wachungaji hawana akiliwala hawamuulizi Mwenyezi Mungu,hivyo hawastawina kundi lao lote la kondoo limetawanyika.22Sikilizeni! Taarifa inakuja:ghasia kubwa kutoka nchi ya kaskazini!Hii itafanya miji ya Yuda ukiwa,na kuwa makao ya mbweha.
Maombi ya Yeremia
23Ninajua, Ee Mwenyezi Mungu, kwamba maisha ya mwanadamu si yake mwenyewe;hawezi kuziongoza hatua zake mwenyewe.24Unirudi, Ee Mwenyezi Mungu, lakini kwa kipimo cha haki:si katika hasira yako,usije ukaniangamiza.25Umwage ghadhabu yako juu ya mataifawasiokujua wewe,juu ya mataifa wasioliitia jina lako.Kwa kuwa wamemwangamiza Yakobo;wamemwangamiza kabisana kuiharibu nchi yake.