1Ee Mwenyezi Mungu, wewe ni Mungu wangu,nitakutukuza na kulisifu jina lako,kwa maana katika ukamilifu wa uaminifuumetenda mambo ya ajabu,mambo yaliyokusudiwa tangu zamani.2Umeufanya mji kuwa lundo la kifusi,mji wenye ngome kuwa magofu,ngome imara ya wageni kuwa si mji tena,wala hautajengwa tena kamwe.3Kwa hiyo mataifa yenye nguvu yatakuheshimu,miji ya mataifa katili itakuogopa wewe.4Umekuwa kimbilio la watu maskini,kimbilio la mhitaji katika taabu yake,hifadhi wakati wa dhorubana kivuli wakati wa hari.Kwa maana pumzi ya wakatilini kama dhoruba ipigayo ukuta5na kama joto la jangwani.Wewe wanyamazisha kelele ya wageni;kama vile hari ipunguzwavyo na kivuli cha wingu,ndivyo wimbo wa wakatili unyamazishwavyo.6Juu ya mlima huu Mwenyezi Mungu, Mungu wa majeshi ya mbinguni ataandaakaramu ya vinono kwa mataifa yote,karamu ya mvinyo wa zamani,nyama nzuri sana na divai zilizo bora sana.7Juu ya mlima huu ataharibusitara ihifadhiyo mataifa yote,kile kifuniko kifunikacho mataifa yote,8yeye atameza mauti milele.Bwana Mungu Mwenyezi atafuta machozi katika nyuso zote;ataondoa aibu ya watu wake duniani kote.Mwenyezi Mungu amesema hili.9Katika siku ile watasema,“Hakika huyu ndiye Mungu wetu;tulimtumaini, naye akatuokoa.Huyu ndiye Mwenyezi Mungu, tuliyemtumaini;sisi tushangilie na kufurahia katika wokovu wake.”10Mkono wa Mwenyezi Mungu utatulia juu ya mlima huu,bali Moabu atakanyagwa chinikama majani makavu yakanyagwavyo kwenye shimo la mbolea.11Watakunjua mikono yao katikati yake,kama vile mwogeleaji akunjuavyo mikono yake ili aogelee.Mungu atashusha kiburi chaolicha ya ujanja wa mikono yao.12Atabomoa kuta ndefu za ngome yakona kuziangusha chini,atazishusha chini ardhini,hadi mavumbini kabisa.