Isaya18swh_onmm

Unabii dhidi ya Kushi

1Ole kwa nchi ya mvumo wa mabawa ,kando ya mito ya Kushi,2iwapelekayo wajumbe wake kupitia baharikwa mashua za mafunjo juu ya maji.Nendeni, wajumbe wepesi,kwa taifa la watu warefu wenye ngozi nyororo,kwa taifa linaloogopwa mbali na karibu,taifa gomvi lenye lugha ngeni,ambalo nchi yao imegawanywa kwa mito.
3Enyi mataifa yote ya ulimwengu,ninyi mnaoishi dunianiwakati bendera itakapoinuliwa milimani,mtaiona,nayo tarumbeta itakapolia,mtaisikia.4Hili ndilo Mwenyezi Mungu aliloniambia:“Nitatulia kimya na kutazamakutoka maskani yangu,kama joto linalometameta katika mwanga wa jua,kama wingu la umandekatika joto la wakati wa mavuno.”5Kwa maana, kabla ya mavuno,wakati wa kuchanua ukishapitana maua yakawa zabibu zinazoiva,atayakata machipukizi kwa mundu wa kupogolea matawi,naye atakata na kuyaondoa matawi yaliyopanuka.6Yote yataachwa kwa ajili ya ndege wawindao wa mlimanina wanyama pori,ndege watajilisha juu yake wakati wote wa kiangazi,nao wanyama pori wakati wote wa masika.7Wakati huo matoleo yataletwa kwa Mwenyezi Mungu, Mungu wa majeshi ya mbingunikutoka kwa taifa la watu warefu wenye ngozi nyororo,kutoka kwa taifa linaloogopwa mbali na karibu,kutoka taifa gomvi lenye lugha ngeni,ambalo nchi yao imegawanywa kwa mito,matoleo yataletwa katika Mlima Sayuni, mahali pa Jina la Mwenyezi Mungu, Mungu wa majeshi ya mbinguni.