Isaya12swh_onmm

Kushukuru na kusifu

1Katika siku ile utasema:“Nitakusifu wewe, Ee Mwenyezi Mungu.Ingawa ulinikasirikia,hasira yako imegeukia mbalinawe umenifariji.2Hakika Mungu ni wokovu wangu;nitamtumaini wala sitaogopa.Mwenyezi Mungu, Mwenyezi Mungu,ni nguvu zangu na wimbo wangu;amekuwa wokovu wangu.”3Kwa furaha mtachota majikutoka visima vya wokovu.4Katika siku hiyo mtasema:“Mshukuruni Mwenyezi Mungu, mliitie jina lake;julisheni miongoni mwa mataifa yale aliyoyafanya,tangazeni kuwa jina lake limetukuka.5Mwimbieni Mwenyezi Mungu, kwa kuwa ametenda mambo makuu,hili na lijulikane duniani kote.6Pazeni sauti mwimbe kwa furaha, watu wa Sayuni,kwa maana mkuu ni yeye Aliye Mtakatifu wa Israeli miongoni mwenu.”