1Chipukizi litatokea kutoka shina la Yese,kutoka mizizi yake Tawi litazaa tunda.2Roho wa Mwenyezi Mungu atakaa juu yake,Roho wa hekima na wa ufahamu,Roho wa shauri na wa uweza,Roho wa maarifa na wa kumcha Mwenyezi Mungu3naye atafurahia kumcha Mwenyezi Mungu.Hatahukumu kwa yale ayaonayo kwa macho yake,wala kuamua kwa yale ayasikiayo kwa masikio yake,4bali kwa uadilifu atahukumu wahitaji,kwa haki ataamua wanyenyekevu wa dunia.Ataipiga dunia kwa fimbo ya kinywa chake,kwa pumzi ya midomo yake atawaua waovu.5Haki itakuwa mkanda wakena uaminifu utakuwa mshipi kiunoni mwake.6Mbwa-mwitu ataishi pamoja na mwana-kondoo,naye chui atalala pamoja na mbuzi,ndama, mwana simba na ng’ombe wa mwaka mmojawatakaa pamoja,naye mtoto mdogo atawaongoza.7Ng’ombe na dubu watalisha pamoja,watoto wao watalala pamoja,na simba atakula majani makavu kama maksai.8Mtoto mchanga atacheza karibu na shimo la nyoka,naye mtoto mdogo ataweka mkono wakekwenye kiota cha fira.9Hawatadhuru wala kuharibujuu ya mlima wangu mtakatifu wote,kwa kuwa dunia itajawa na kumjua Mwenyezi Mungukama maji yajazavyo bahari.10Katika siku hiyo, Shina la Yese atasimama kama bendera kwa ajili ya mataifa. Mataifa yatakusanyika kwake, na mahali pake pa kupumzikia patakuwa utukufu.11Katika siku hiyo Bwana atanyoosha mkono wake mara ya pili kurudisha mabaki ya watu wake waliosalia kutoka Ashuru, Misri, Pathrosi, Kushi, Elamu, Babeli, Hamathi, na kutoka visiwa vya baharini.12Atainua bendera kwa mataifana kuwakusanya Waisraeli walio uhamishoni;atawakusanya watu wa Yuda waliotawanyikakutoka pembe nne za dunia.13Wivu wa Efraimu utatoweka,na adui wa Yuda watakatiliwa mbali;Efraimu hatamwonea Yuda wivu,wala Yuda hatakuwa na uadui na Efraimu.14Watawashukia katika miteremko ya Wafilistihadi upande wa magharibi,kwa pamoja watawateka watu nyarahadi upande wa mashariki.Watawapiga Edomu na Moabu,na Waamoni watatawaliwa nao.15Mwenyezi Mungu atakaushaghuba ya bahari ya Misri;kwa upepo mkavu ataupeleka mkono wakejuu ya Mto Frati.Ataugawanya katika vijito sabaili watu waweze kuuvuka wakiwa wamevaa viatu.16Kutakuwa na njia kuu kwa mabaki ya watu wakewale waliosalia kutoka Ashuru,kama ilivyokuwa kwa Israeliwalipopanda kutoka Misri.