Isaya10swh_onmm
1Ole wao wawekao sheria zisizo za haki,kwa wale watoao amri za kuonea,2kuwanyima maskini haki zaona kuzuilia haki za watu wangu waliodhulumiwa,kuwafanya wajane mawindo yaona kuwanyang’anya yatima.3Mtafanya nini siku ya hukumu,wakati maafa yatakapokuja kutoka mbali?Mtamkimbilia nani awape msaada?Mtaacha wapi mali yenu?4Hakutasalia kitu chochote,isipokuwa kujikunyata miongoni mwa mateka,au kuanguka miongoni mwa waliouawa.Hata kwa haya yote, hasira yake haijageukia mbali,mkono wake bado umeinuliwa juu.