Hosea7swh_onmm
1kila mara nilipotaka kumponya Israeli,dhambi za Efraimu zinafichuliwana maovu ya Samaria yanafunuliwa.Wanafanya udanganyifu,wezi huvunja nyumba,maharamia hunyang’anya barabarani,2lakini hawafahamu kwambaninakumbuka matendo yao yote mabaya.Dhambi zao zimewameza,ziko mbele zangu siku zote.3“Wanamfurahisha sana mfalme kwa maovu yao,wakuu wao kwa uongo wao.4Wote ni wazinzi,wanawaka kama tanuruambalo moto wake mwokaji hana haja ya kuuchocheakuanzia kukanda ungahadi umekwisha kuumuka.5Katika sikukuu ya mfalme wetuwakuu wanawaka kwa mvinyo,naye anawaunga mkono wenye mizaha.6Mioyo yao ni kama tanuru,wanamwendea kwa hila.Hasira yao inafoka moshi usiku kucha,wakati wa asubuhi inalipukakama miali ya moto.7Wote ni moto kama tanuru;wanawaangamiza watawala wao.Wafalme wake wote wanaanguka,wala hakuna yeyote kati yao aniitaye mimi.8“Efraimu anajichanganya na mataifa;Efraimu ni mkate ambao haukuiva.9Wageni wananyonya nguvu zake,lakini hafahamu hilo.Nywele zake zina mvi hapa na pale,lakini hana habari.10Kiburi cha Israeli kinashuhudia dhidi yake,lakini pamoja na haya yoteharudi kwa Mwenyezi Mungu, Mungu wake,wala kumtafuta.11“Efraimu ni kama hua,hudanganywa kwa urahisi na hana akili:mara anaita Misri,mara anageukia Ashuru.12Watakapoenda, nitatupa wavu wangu juu yao;nitawavuta chini waanguke kama ndege wa angani.Nitakaposikia wakikusanyika pamoja,nitawanasa.13Ole wao, kwa sababuwamepotoka kutoka kwangu!Maangamizi ni yaokwa sababu wameniasi!Ninatamani kuwakomboa,lakini wanasema uongo dhidi yangu.14Hawanililii mimi kutoka mioyoni mwao,bali wanaomboleza vitandani mwao.Hukusanyika pamoja kwa ajili ya nafaka na divai mpya,lakini hugeukia mbali nami.15Niliwafundisha na kuwatia nguvu,lakini wanapanga mabaya dhidi yangu.16Hawamgeukii Yeye Aliye Juu Sana,wako kama upinde wenye kasoro.Viongozi wao wataanguka kwa upangakwa sababu ya maneno yao ya jeuri.Kwa ajili ya hili watadhihakiwakatika nchi ya Misri.