Hosea6swh_onmm

Israeli asiye tubu

1“Njooni, tumrudie Mwenyezi Mungu.Ameturarua vipande vipandelakini atatuponya;ametujeruhi lakiniatatufunga majeraha yetu.2Baada ya siku mbili atatufufua;katika siku ya tatu atatuinua,ili tuweze kuishi mbele zake.3Tumkubali Mwenyezi Mungu,tukaze kumkubali yeye.Kutokea kwake ni hakika kama vilekuchomoza kwa jua;atatujia kama mvua za masika,kama vile mvua za vuliziinyweshavyo nchi.”
4“Nifanye nini nawe, Efraimu?Nifanye nini nawe, Yuda?Upendo wako ni kama ukungu wa asubuhi,kama umande wa alfajiri utowekao.5Kwa hiyo nimewakata ninyi vipande vipandenikitumia manabii wangu;nimewaua ninyi kwa maneno ya kinywa changu,hukumu zangu zinawakakama umeme juu yenu.6Kwa maana nataka rehema, wala si dhabihu,na kumkubali Mungukuliko sadaka za kuteketezwa.7Wamevunja agano kama Adamu:hawakuwa waaminifu kwangu huko.8Gileadi ni mji wa watenda maovu,umetiwa madoa kwa nyayo za damu.9Kama wanyang’anyi wamviziavyo mtu,ndivyo magenge ya makuhani wafanyavyo;wanaulia watu kwenye njia iendayo Shekemu,wakifanya uhalifu wa aibu.10Nimeona jambo la kutishakatika nyumba ya Israeli.Huko Efraimu amejitolea kwa ukahabana Israeli amenajisika.
11“Pia kwa ajili yako, Yuda,mavuno yameamriwa.“Wakati wowote ningerejesha neema ya watu wangu,