1Sikieni neno la Mwenyezi Mungu, enyi Waisraeli,kwa sababu Mwenyezi Mungu analo shtakadhidi yenu ninyi mnaoishi katika nchi:“Hakuna uaminifu, hakuna upendo,hakuna kumjua Mungu katika nchi.2Kuna kulaani tu, uongo na uuaji,wizi na uzinzi,bila kuwa na mipaka,nao umwagaji damu mmojabaada ya mwingine.3Kwa sababu hii nchi huomboleza,wote wanaoishi ndani yake wanadhoofika;wanyama wa kondeni, ndege wa anganina samaki wa baharini wanakufa.4“Lakini mtu yeyote na asilete shtaka,mtu yeyote na asimlaumu mwenzake,kwa maana watu wako ni kama walewaletao mashtaka dhidi ya kuhani.5Unajikwaa usiku na mchana,nao manabii hujikwaa pamoja nawe.Kwa hiyo nitamwangamiza mama yako:6watu wangu wanaangamizwakwa kukosa maarifa.“Kwa kuwa wewe umeyakataa maarifa,mimi nami nitakukataa weweusiwe kuhani kwangu mimi;kwa kuwa umeacha kuijali Torati ya Mungu wakomimi nami sitawajali watoto wako.7Kadiri makuhani walivyoongezeka,ndivyo walivyozidi kutenda dhambi dhidi yangu,walibadilisha utukufu wao kwa kitu cha aibu.8Wanajilisha dhambi za watu wanguna kupendezwa na uovu wao.9Hata itakuwa: Kama walivyo watu,ndivyo walivyo makuhani.Nitawaadhibu wote wawili kwa ajili ya njia zaona kuwalipa kwa matendo yao.10“Watakula lakini hawatashiba;watajiingiza katika ukahabalakini hawataongezeka,kwa sababu wamemwacha Mwenyezi Munguna kujiingiza wenyewe11katika ukahaba;kunywa divai ya zamani na divai mpyahuondoa ufahamu12wa watu wangu.Hutaka shauri kutoka kwa sanamu ya mtinao hujibiwa na fimbo ya mti.Roho ya ukahaba imewapotosha,hawana uaminifu kwa Mungu wao.13Wanatoa dhabihu juu ya vilele vya milimana sadaka za kuteketezwa juu ya vilima,chini ya mialoni, milibua na miela,ambako kuna vivuli vizuri.Kwa hiyo binti zenu wamegeukia ukahabana wake za wana wenu uzinzi.14“Sitawaadhibu binti zenu wakatiwanapogeukia ukahaba,wala wake za wana wenuwanapofanya uzinzi,kwa sababu wanaume wenyewe huandamana na malayana kutambikia pamoja na makahabawa mahali pa ibada za sanamu:watu wasiokuwa na ufahamuwataangamia!15“Ingawa umefanya uzinzi, ee Israeli,Yuda naye asije akawa na hatia.“Usiende Gilgali,usipande kwenda Beth-Aveni .Wala usiape,‘Hakika kama Mwenyezi Mungu aishivyo!’16Waisraeli ni wakaidi,kama ndama jike mkaidi.Ni jinsi gani basi Mwenyezi Mungu anaweza kuwachungakama wana-kondookatika shamba la majani?17Efraimu amejiunga na sanamu,achana naye!18Hata wakati wamemaliza vileo vyaowanaendelea na ukahaba wao,watawala wao hupenda sananjia za aibu.19Kisulisuli kitawafagilia mbalina dhabihu zao zitawaletea aibu.