1“Waambie ndugu zako, ‘Watu wangu,’ na pia waambie dada zako, ‘Wapendwa wangu.’
Israeli kuadhibiwa na kurudishwa
2“Mkemeeni mama yenu, mkemeeni,kwa maana yeye si mke wangu,nami si mume wake.Aondoe sura ya uzinzi katika uso wakena uzinzi kati ya matiti yake.3Kama sivyo nitamvua nguo zake awe uchina kumwacha uchi kama siku ile aliyozaliwa.Nitamfanya kama jangwa,nitamgeuza awe nchi ya kiu,nami nitamuua kwa kiu.4Sitaonesha upendo wangu kwa watoto wake,kwa sababu ni watoto wa uzinzi.5Mama yao amekosa uaminifuna amewachukua mimba katika aibu.Gomeri alisema, ‘Nitawaendea wapenzi wangu,ambao hunipa chakula changuna maji yangu,sufu yangu na kitani yangu, mafuta yanguna kinywaji changu.’6Kwa hiyo mimi Mungu nitaizuia njia yakekwa vichaka vya miiba,nitamjengea ukuta iliasiweze kutoka.7Gomeri atawafuatia wapenzi wake lakini hatawapata;atawatafuta lakini hatawapata.Kisha atasema,‘Nitarudi kwa mume wangu kama kwanza,kwa maana nilikuwa na hali njemakuliko sasa.’8Gomeri hajakubali kuwa mimi ndiyeniliyempa nafaka, divai mpya na mafuta,niliyemwongezea fedha na dhahabu waliyoitumiakwa kumtumikia Baali.9“Kwa hiyo nitachukua nafaka yangu wakati itakapokomaana divai yangu mpya wakati itakapokuwa tayari.Nitamnyang’anya sufu yangu na kitani yanguiliyokusudiwa kufunika uchi wake.10Basi sasa nitaufunua ufisadi wakembele ya wapenzi wake;hakuna yeyote atakayemtoamikononi mwangu.11Nitakomesha furaha na macheko yake yote:sikukuu zake za mwaka,sikukuu za Miandamo ya Mwezi,siku zake za Sabato,sikukuu zake zote zilizoamriwa.12Nitaiharibu mizabibu yake na mitini yake,ambayo alisema yalikuwa malipo yakekutoka kwa wapenzi wake;nitaifanya kuwa kichaka,nao wanyama pori wataila.13Nitamwadhibu kwa ajili ya sikualizowafukizia uvumba Mabaali;alipojipamba kwa petena kwa vito vya thamani,na kuwaendea wapenzi wake,lakini mimi alinisahau,”asema Mwenyezi Mungu.14“Kwa hiyo sasa nitamshawishi;nitamwongoza hadi jangwanina kuzungumza naye kwa upole.15Huko nitamrudishia mashamba yake ya mizabibu,nami nitalifanya Bonde la Akorimlango wa matumaini.Huko ataimba kama alivyofanya katika siku za ujana wake,kama siku zile alizotoka Misri.16“Katika siku ile,” asema Mwenyezi Mungu,“utaniita mimi ‘Mume wangu ’;hutaniita tena mimi ‘Bwana wangu .’17Nitaondoa majina ya Mabaali kutoka mdomoni mwake,wala hataomba tena kwa majina yao.18Katika siku ile nitafanya agano kwa ajili yaona wanyama wa kondeni, na ndege wa angani,na viumbe vinavyotambaa ardhini.Upinde, upanga na vita,nitaondolea mbali katika nchi,ili wote waweze kukaa salama.19Nitakuposa uwe wangu milele;nitakuposa kwa uadilifu na haki,kwa upendo na huruma.20Nitakuposa kwa uaminifu,nawe utamkubali Mwenyezi Mungu.21“Katika siku ile nitajibu,”asema Mwenyezi Mungu,“nitajibu kwa anga,nazo anga zitajibu kwa nchi;22nayo nchi itajibu kwa nafaka,divai mpya na mafuta,navyo vitajibu kwa Yezreeli.23Nitampanda katika nchi kwa ajili yangu mwenyewe;nami nitaonesha pendo langu kwakeyule ambaye nilimwita, ‘Si Mpendwa Wangu .’Nitawaambia wale walioitwa, ‘Sio Watu Wangu ,’‘Ninyi ni Watu Wangu’;nao watasema, ‘Wewe ndiwe Mungu wangu’.”