Hosea13swh_onmm

Hasira ya Mwenyezi Mungu dhidi ya Israeli

1Efraimu alipozungumza, watu walitetemeka;alitukuzwa katika Israeli.Lakini alikuwa na hatia ya kumwabudu Baali,naye akafa.2Sasa wanatenda dhambi zaidi na zaidi;wanajitengenezea sanamukutokana na fedha yao,vinyago vilivyotengenezwa kwa uhodari,vyote kazi ya fundi stadi.Inasemekana kuhusu hawa watu,“Hutoa dhabihu za binadamuna kubusu sanamu za ndama.”3Kwa hiyo watakuwa kama ukungu wa asubuhi,kama umande wa alfajiri utowekao,kama makapi yapeperushwayokutoka sakafu ya kupuria nafaka,kama moshi utorokao kupitia dirishani.
4“Bali mimi ndimi Mwenyezi Mungu, Mungu wenu,niliyewaleta ninyi toka Misri.Msimkubali Mungu mwingine ila mimi,hakuna Mwokozi isipokuwa mimi.5Niliwatunza huko jangwani,katika nchi yenye joto liunguzalo.6Nilipowalisha, walishiba,waliposhiba, wakajivuna,kisha wakanisahau mimi.7Kwa hiyo nitakuja juu yao kama simba,kama chui nitawavizia kando ya njia.8Kama dubu aliyenyang’anywa watoto wake,nitawashambulia na kurarua vifua vyenu.Kama simba nitawala;mnyama pori atawararua vipande vipande.
9“Ee Israeli, umeangamizwa,kwa sababu wewe u kinyume nami,kinyume na msaidizi wako.10Yuko wapi mfalme wako,ili apate kukuokoa?Wako wapi watawala wako katika miji yako yoteambao ulisema kuwahusu,‘Nipe mfalme na wakuu’?11Hivyo katika hasira yangu nilikupa mfalmena katika ghadhabu yangu nilimwondoa.12Kosa la Efraimu limehifadhiwa,dhambi zake zimewekwa katika kumbukumbu.13Uchungu kama wa mwanamke anayejifungua mtoto humjia,lakini yeye ni mtoto asiyekuwa na hekima;wakati utakapowadia hatatokakatika tumbo la mama yake.
14“Nitawakomboa watu hawa kutoka nguvu za kaburi,nitawakomboa kutoka mautini.Yako wapi, ee mauti, mateso yako?Uko wapi, ee Kuzimu , uharibifu wako?“Sitakuwa na huruma,15hata ingawa Efraimu atastawimiongoni mwa ndugu zake.Upepo wa mashariki kutoka kwa Mwenyezi Mungu utakuja,ukivuma kutoka jangwani,chemchemi yake haitatoa majina kisima chake kitakauka.Ghala lake litatekwahazina zake zote.16Watu wa Samaria ni lazima wabebe hatia yao,kwa sababu wameasi dhidi ya Mungu wao.Wataanguka kwa upanga;watoto wao wadogo watatupwa kwa nguvu ardhini,wanawake wao walio na mimba watatumbuliwa.”