Hosea12swh_onmm

1Efraimu anajilisha upepo;hufukuzia upepo wa mashariki kutwa nzimana kuzidisha uongo na jeuri.Anafanya mkataba na Ashuruna kutuma mafuta ya zeituni Misri.2Mwenyezi Mungu analo shtaka dhidi ya Yuda,atamwadhibu Yakobo kwa kadiri ya njia zakena kumlipa kwa kadiri ya matendo yake.3Yakobo akiwa tumboni alishika kisigino cha kaka yake;kama mwanadamu, alishindana na Mungu.4Alishindana na malaika na kumshinda;alilia na kuomba upendeleo wake.Alimkuta huko Bethelina kuzungumza naye huko:5Bwana Mwenyezi Mungu,Mungu wa majeshi ya mbinguni,Mwenyezi Mungu ndilo jina lake!6Lakini ni lazima urudi kwa Mungu wako;dumisha upendo na haki,nawe umngojee Mungu wako siku zote.
7Mfanyabiashara hutumia vipimo vya udanganyifu;hupenda kupunja.8Efraimu hujisifu akisema,“Mimi ni tajiri sana; nimetajirika.Pamoja na utajiri wangu wote hawatakuta ndani yanguuovu wowote au dhambi.”
9“Mimi ndimi Mwenyezi Mungu, Mungu wenu,niliyewaleta kutoka Misri;nitawafanya mkae tena kwenye mahema,kama vile katika sikuza sikukuu zenu zilizoamriwa.10Niliongea na manabii, nikawapa maono mengina kusema mifano kupitia wao.”
11Je, Gileadi si mwovu?Watu wake hawafai kitu!Je, hawatoi dhabihu za mafahali huko Gilgali?Madhabahu zao zitakuwakama malundo ya mawekatika shamba lililolimwa.12Yakobo alikimbilia katika nchi ya Aramu;Israeli alitumika ili apate mke,ili aweze kulipa kwa ajili yake alichunga kondoo.13Mwenyezi Mungu alimtumia nabiikumpandisha Israeli kutoka Misri,kupitia kwa nabii alimtunza.14Lakini Efraimu amemchochea sana hasira;Bwana wake ataleta juu yakehatia yake ya kumwaga damu naye atamlipizakwa ajili ya dharau yake.