1“Israeli alipokuwa mtoto, nilimpenda;nilimwita mwanangu kutoka Misri.2Lakini kadiri nilivyomwita Israeli,ndivyo walivyoenda mbali nami.Walitoa dhabihu kwa Mabaalina kufukiza uvumba kwa vinyago.3Mimi ndiye niliyemfundisha Efraimu kutembea,nikiwashika mikono;lakini hawakutambuakuwa ni mimi niliyewaponya.4Niliwaongoza kwa kamba za huruma ya kibinadamu,kwa vifungo vya upendo;niliondoa nira shingoni mwaonami nikainama kuwalisha.5“Je, hawatarudi Misri,nayo Ashuru haitawatawalakwa sababu wamekataa kutubu?6Upanga utavurumishwa katika miji yao,nao utaharibu makomeo ya malango yaona kukomesha mipango yao.7Watu wangu wamedhamiria kuniacha.Hata wakimwita Yeye Aliye Juu Sana,kwa vyovyote hatawainua.8“Efraimu, ninawezaje kukuacha?Ee Israeli, ninawezaje kukutoa?Nitawezaje kukutendea kama Adma?Nitawezaje kukufanya kama Seboimu?Moyo wangu umegeuka ndani yangu,huruma zangu zote zimeamshwa.9Sitatimiza hasira yangu kali,wala sitageuka na kumharibu Efraimu.Kwa kuwa mimi ndimi Mungu,wala si mwanadamu,Aliye Mtakatifu miongoni mwenu.Sitakuja kwa ghadhabu.10Watamfuata Mwenyezi Mungu;atanguruma kama simba.Anaponguruma,watoto wake watakuja wakitetemekakutoka magharibi.11Watakuja wakitetemekakama ndege wakitoka Misri,kama hua wakitoka Ashuru.Nitawafanya waishi katika nyumba zao,”asema Mwenyezi Mungu.
Dhambi ya Israeli
12Efraimu amenizunguka kwa uongo,nyumba ya Israeli kwa udanganyifu.Naye Yuda ni mkaidi dhidi ya Mungu,hata kinyume cha yule mwaminifu Aliye Mtakatifu.