Hosea10swh_onmm
1Israeli alikuwa mzabibu uliostawi sana,alijizalia matunda mwenyewe.Kadiri matunda yake yalivyoongezeka,alijenga madhabahu zaidi;kadiri nchi yake ilivyostawi,alipamba mawe yake ya ibada.2Moyo wao ni mdanganyifu,nao sasa lazima wachukue hatia yao.Mwenyezi Mungu atabomoa madhabahu zaona kuharibu mawe yao ya ibada.3Kisha watasema, “Hatuna mfalmekwa sababu hatukumheshimu Mwenyezi Mungu.Lakini hata kama tungekuwa na mfalme,angeweza kutufanyia nini?”4Wanaweka ahadi nyingi,huapa viapo vya uongowanapofanya mapatano;kwa hiyo mashtaka huchipukakama magugu ya sumukatika shamba lililolimwa.5Watu wanaoishi Samaria huogopakwa ajili ya sanamu ya ndama ya Beth-Aveni .Watu wake wataiombolezea,vivyo hivyo kuhani wake wa kuabudu sanamu,wale waliokuwa wamefurahia fahari yake,kwa sababu itaondolewa kutoka kwaokwenda uhamishoni.6Itachukuliwa kwenda Ashurukama ushuru kwa mfalme mkuu.Efraimu atafedheheshwa;Israeli ataaibika kwa ajili ya sanamu zake za mti.7Samaria na mfalme wake wataeleakama kijiti juu ya maji.8Mahali pa juu pa uovu pataharibiwa:ndiyo dhambi ya Israeli.Miiba na mibaruti itaotana kufunika madhabahu zao.Kisha wataiambia milima, “Tufunikeni!”na vilima, “Tuangukieni!”9“Tangu siku za Gibea, umetenda dhambi, ee Israeli,huko ndiko ulibaki.Je, vita havikuwapatawatenda maovu huko Gibea?10Wakati nitakapopenda, nitawaadhibu;mataifa yatakusanywa dhidi yaoili kuwaweka katika vifungokwa ajili ya dhambi zao mbili.11Efraimu ni ndama jike aliyefundishwaambaye hupenda kupura;hivyo nitamfunga nirajuu ya shingo yake nzuri.Nitamwendesha Efraimu,Yuda lazima alime,naye Yakobo lazima avunjavunjemabonge ya udongo.12Jipandieni wenyewe haki,vuneni matunda ya upendo usio na kikomo,vunjeni ardhi yenu isiyolimwa;kwa kuwa ni wakati wa kumtafuta Mwenyezi Mungu,hadi atakapokujana kuwanyeshea juu yenu haki.13Lakini mmepanda uovu,mkavuna ubaya,mmekula tunda la udanganyifu.Kwa sababu mmetegemea nguvu zenu wenyewena wingi wa mashujaa wenu,14mngurumo wa vita utainuka dhidi ya watu wako,na ngome zako zote zitaharibiwa:kama Shalmani alivyoharibu Beth-Arbeli katika siku ile ya vita,wakati mama pamoja na watoto waowalipotupwa kwa nguvu ardhini.15Ndivyo itakavyotokea kwako, ee Betheli,kwa sababu uovu wako ni mkuu.Siku ile itakapopambazuka,mfalme wa Israeli ataharibiwa kabisa.