Waebrania5swh_onmm
1Kwa maana kila kuhani mkuu anayechaguliwa miongoni mwa wanadamu anawekwa kuwawakilisha kwa mambo yanayomhusu Mungu, ili apate kutoa matoleo na dhabihu kwa ajili ya dhambi.2Kwa kuwa yeye mwenyewe ni dhaifu, aweza kuwachukulia kwa upole wale wasiojua na kupotoka.3Hii ndiyo sababu inampasa kutoa dhabihu kwa ajili ya dhambi zake mwenyewe na vivyo hivyo kwa ajili ya dhambi za watu.4Hakuna anayejitwalia heshima hii mwenyewe; ni lazima aitwe na Mungu, kama vile Haruni alivyoitwa.5Pia Al-Masihi hakujitwalia utukufu yeye mwenyewe wa kuwa Kuhani Mkuu, bali Mungu alimwambia,“Wewe ni Mwanangu;leo mimi nimekuwa Baba yako.”6Pia mahali pengine asema,“Wewe ni kuhani milele,kwa mfano wa Melkizedeki.”7Katika siku za maisha ya Isa hapa duniani, alimtolea maombi na dua pamoja na kulia sana na machozi, yeye awezaye kumwokoa na mauti, naye Mungu akamsikia kwa sababu ya kutii kwake kwa unyenyekevu.8Ingawa alikuwa Mwana, alijifunza utiifu kutokana na mateso aliyoyapata,9naye akiisha kukamilishwa, akawa chanzo cha wokovu wa milele kwa wote wanaomtii.10Naye amewekwa na Mungu kuwa Kuhani Mkuu kwa mfano wa Melkizedeki.