Wagalatia1
Salamu
1Paulo mtume, si mtume wa wanadamu wala aliyetumwa na mwanadamu, bali na Isa Al-Masihi na Mungu Baba Mwenyezi aliyemfufua Isa kutoka kwa wafu,2na ndugu wote walio pamoja nami.Kwa makundi ya waumini wa Galatia.3Neema na amani zitokazo kwa Mungu, Baba yetu, na kwa Bwana wetu Isa Al-Masihi ziwe nanyi,4yeye aliyejitoa kwa ajili ya dhambi zetu ili apate kutuokoa katika ulimwengu huu wa sasa ulio mbaya, sawasawa na mapenzi yake yeye aliye Mungu na Baba yetu.5Utukufu una yeye milele na milele. Amen.