Ezekieli7swh_onmm

Mwisho umewadia

1Neno la Mwenyezi Mungu likanijia kusema:2“Mwanadamu, hili ndilo asemalo Bwana Mungu Mwenyezi kwa nchi ya Israeli:“ ‘Mwisho! Mwisho umekujajuu ya pembe nne za nchi!3Sasa mwisho umekuja juu yenu,nami nitamwaga hasira yangu dhidi yenu.Nitawahukumu sawasawa na matendo yenuna kuwalipiza kwa ajili ya desturi zenu zote za kuchukiza.4Sitawaonea hurumawala kuwarehemu.Hakika nitawalipiza kwa ajili ya matendo yenuna desturi za machukizo miongoni mwenu.Ndipo mtajua kuwa Mimi ndimi Mwenyezi Mungu.’
5“Hili ndilo asemalo Bwana Mungu Mwenyezi:“ ‘Maafa! Maafa ambayo hayajasikiwa!Tazama, yanakuja!6Mwisho umewadia!Mwisho umewadia!Umejiinua wenyewe dhidi yenu.Tazama, umewadia!7Maangamizi yamekuja juu yenu,ninyi mnaoishi katika nchi.Wakati umewadia! Siku imekaribia!Kuna hofu kuu ya ghafula juu ya milima, wala si furaha.8Ninakaribia kumwaga ghadhabu yangu juu yenuna kumaliza hasira yangu dhidi yenu.Nitawahukumu sawasawa na matendo yenuna kuwalipiza kwa ajili ya desturi zenu zote za machukizo.9Sitawaonea hurumawala kuwarehemu.Nitawalipiza kwa ajili ya matendo yenuna desturi za machukizo miongoni mwenu.“ ‘Ndipo mtajua kuwa Mimi ndimi Mwenyezi Mungu ambaye huwapiga.10“ ‘Tazama, siku imefika!Tazama, imewadia!Maangamizi yamezuka ghafula,fimbo imechanua,nayo majivuno yamechipua!11Jeuri imeinukakuwa fimbo ya kuadhibu waovu.Hakuna hata mmoja wa hao watu atakayeachwa,hata mmoja wa kundi hilo:hakuna utajiri wao utabaki,wala chochote cha thamani.12Wakati umewadia,siku imefika.Mnunuzi na asifurahiwala muuzaji asihuzunike,kwa maana ghadhabu iko juu ya kundi lote.13Muuzaji hatajipatia tenaardhi aliyoiuzawakati wote wawili wangali hai.Kwa kuwa maono kuhusu kundi lotehayatatanguka.Kwa sababu ya dhambi zao, hakuna hata mmojaatakayeokoa maisha yake.
14“ ‘Wajapopiga tarumbetana kuweka kila kitu tayari,hakuna hata mmoja atakayeenda vitani,kwa maana ghadhabu yangu iko juu ya kundi lote.15Nje ni upanga,ndani ni tauni na njaa.Walio shambaniwatakufa kwa upanga,nao waliomo mjininjaa na tauni vitawala.16Wote watakaoponana kutoroka watakuwa milimani,wakiomboleza kama hua wa mabondeni,kila mmoja kwa sababu ya dhambi zake.17Kila mkono utalegeana kila goti litakuwa dhaifu kama maji.18Watavaa guniana kufunikwa na hofu.Nyuso zao zitafunikwa na aibu,na vichwa vyao vitanyolewa.
19“ ‘Watatupa fedha yao barabarani,nayo dhahabu yao itakuwa najisi.Fedha yao na dhahabu yaohavitaweza kuwaokoakatika siku hiyo ya ghadhabu ya Mwenyezi Mungu.Hawatashibisha njaa yaoau kujaza tumbo zao kwa hiyo fedha wala dhahabu,kwa sababu imewaponza wajikwae dhambini.20Walijivunia vito vyao vizurina kuvitumia kutengeneza sanamu za machukizona vinyago vya upotovu.Kwa hiyo nitavifanya vitu hivyo kuwa najisi kwao.21Nitavitia vyote mikononi mwa wagenikuwa nyara na kuwa vitu vilivyotekwa mikononi mwa watu waovu wa dunia,nao watavinajisi.22Nitaugeuza uso wangu mbali nao,nao waovu wa dunia watapanajisi mahali pangu pa thamani.Wanyang’anyi watapaingiana kupanajisi.
23“ ‘Andaa minyororo,kwa sababu nchi imejaa umwagaji wa damuna mji umejaa udhalimu.24Nitaleta taifa ovu kuliko yotekumiliki nyumba zao.Nitakomesha kiburi cha wenye nguvuna mahali pao patakatifu patatiwa unajisi.25Hofu ya ghafula itakapokuja,watatafuta amani, lakini haitapatikana.26Maafa juu ya maafa yatakuja,tetesi ya mabaya juu ya tetesi ya mabaya.Watajitahidi kupata maono kutoka kwa nabii;mafundisho ya sheria toka kwa kuhani yatapotea,vivyo hivyo shauri kutoka kwa wazee.27Mfalme ataomboleza,mwana wa mfalme atavikwa kukata tamaa,nayo mikono ya watu wa nchi itatetemeka.Nitawaadhibu kulingana na matendo yao,na kwa kanuni zao wenyewe nitawahukumu.“ ‘Ndipo watajua kwamba Mimi ndimi Mwenyezi Mungu.’ ”