1Katika mwaka wa kumi na mbili, mwezi wa kumi na mbili, siku ya kwanza ya mwezi, neno la Mwenyezi Mungu likanijia, kusema:2“Mwanadamu, fanya maombolezo kwa ajili ya Farao mfalme wa Misri na umwambie:“ ‘Wewe ni kama simba miongoni mwa mataifa,wewe ni kama mnyama mkubwa baharini,unapiga maji kwa kishindo katika vijito vyako,unayavuruga maji kwa miguu yako,na kuchafua vijito.3“ ‘Hili ndilo asemalo Bwana Mungu Mwenyezi:“ ‘Nikiwa pamoja na wingi mkubwa wa watunitautupa wavu wangu juu yako,nao watakukokota katika wavu wangu.4Nitakutupa nchi kavuna kukuvurumisha uwanjani.Nitawafanya ndege wote wa angani watue juu yakona wanyama wote wa nchiwatajishibisha nyama yako.5Nitatawanya nyama yako juu ya milimana kujaza mabonde kwa mabaki yako.6Nitailowanisha nchi kwa damu yako inayotiririkanjia yote hadi milimani,nayo mabonde yatajazwa na nyama yako.7Nitakapokuzimisha, nitafunika mbinguna kuzitia nyota zake giza;nitalifunika jua kwa wingu,nao mwezi hautatoa nuru yake.8Mianga yote itoayo nuru anganinitaitia giza juu yako;nitaleta giza juu ya nchi yako,asema Bwana Mungu Mwenyezi.9Nitaifadhaisha mioyo ya mataifa menginitakapokuangamiza miongoni mwa mataifa,nikikuleta uhamishoni miongoni mwa nchiambazo hujapata kuzijua.10Nitayafanya mataifa mengi wakustaajabie,wafalme wao watatetemekakwa hofu kwa ajili yakonitakapotikisa upanga wangu mbele yao.Siku ya anguko lakokila mmoja wao atatetemekakila dakika kwa ajili ya maisha yake.11“ ‘Kwa kuwa hili ndilo asemalo Bwana Mungu Mwenyezi:“ ‘Upanga wa mfalme wa Babeliutakuja dhidi yako.12Nitayafanya makundi yako kuangukakwa panga za mashujaa:taifa katili kuliko mataifa yote.Watakivunjavunja kiburi cha Misri,nayo makundi yake yote yatashindwa.13Nitaangamiza mifugo yake yotewanaojilisha kando ya maji mengi:hayatavurugwa tena kwa mguu wa mwanadamuwala kwato za mnyamahazitayachafua tena.14Kisha nitafanya maji yake yatuliena kufanya vijito vyakevitiririke kama mafuta,asema Bwana Mungu Mwenyezi.15Nitakapoifanya Misri kuwa ukiwa,na kuiondolea nchi kila kitu kilichomo,nitakapowapiga wote wanaoishi humo,ndipo watajua kuwaMimi ndimi Mwenyezi Mungu.’16“Hili ndilo ombolezo watakalomwimbia. Binti za mataifa wataliimba, kwa kuwa Misri na makundi yake yote wataliimba, asema Bwana Mungu Mwenyezi.”
Misri kuteremka Kuzimu
17Katika mwaka wa kumi na mbili, mwezi wa kwanza, siku ya kumi na tano ya mwezi, neno la Mwenyezi Mungu likanijia kusema:18“Mwanadamu, omboleza kwa ajili ya makundi ya Misri na uwatupe Kuzimu, yeye na binti za mataifa yenye nguvu, waende huko pamoja nao wanaoshuka shimoni.19Je, ninyi mmekubalika zaidi ya wengine? Shukeni chini! Nanyi mkalazwe pamoja na hao wasiotahiriwa!20Wataanguka miongoni mwa wale waliouawa kwa upanga. Upanga umefutwa; mwache aburutwe mbali pamoja na hao watu wake wote.21Kutoka Kuzimu viongozi hodari watanena kuhusu Misri pamoja na wale walioungana nao, ‘Wameshuka chini, nao wamelala kimya pamoja na hao wasiotahiriwa, pamoja na wale waliouawa kwa upanga.’22“Ashuru yuko huko pamoja na jeshi lake lote, amezungukwa na makaburi ya watu wake wote waliouawa, wale wote walioanguka kwa upanga.23Makaburi yao yako kwenye kina cha chini cha shimo na jeshi lake limelala kulizunguka kaburi lake. Wote waliokuwa wameeneza hofu kuu katika nchi ya walio hai wameuawa, wameanguka kwa upanga.24“Elamu yuko huko, pamoja na makundi yake yote wakiwa wamelizunguka kaburi lake. Wote wameuawa, wameanguka kwa upanga. Wote waliokuwa wameeneza hofu katika nchi ya walio hai walishuka Kuzimu bila kutahiriwa. Wanaichukua aibu yao pamoja na wale wanaoshuka shimoni.25Kitanda kimetandikwa kwa ajili yake miongoni mwa waliouawa, pamoja na makundi yake yote wakiwa wamelizunguka kaburi lake. Wote ni watu wasiotahiriwa, wameuawa kwa upanga. Kwa sababu vitisho vyao vilienea katika nchi ya walio hai, wameichukua aibu yao pamoja na wale wanaoshuka shimoni, nao wamewekwa miongoni mwa waliouawa.26“Mesheki na Tubali wako humo, pamoja na makundi yao wakiwa wameyazunguka makaburi yao. Wote hawakutahiriwa, wameuawa kwa upanga kwa sababu walieneza vitisho vyao katika nchi ya walio hai.27Je, hawakulala na mashujaa wengine wasiotahiriwa waliouawa, ambao wameshuka kaburiniwakiwa na silaha zao za vita, ambao panga zao ziliwekwa chini ya vichwa vyao na uovu wao juu ya mifupa yao? Adhabu kwa ajili ya dhambi zao ilikuwa juu ya mifupa yao, ingawa vitisho vya mashujaa hawa vilikuwa vimeenea hadi kwenye nchi ya walio hai.28“Wewe pia, ee Farao, utavunjwa nawe utalala miongoni mwa wasiotahiriwa, pamoja na wale waliouawa kwa upanga.29“Edomu yuko humo, wafalme wake wote na wakuu wake wote, ambao ijapokuwa wana nguvu, wamelazwa pamoja na wale waliouawa kwa upanga. Wamelala pamoja na wasiotahiriwa, pamoja na wale wanaoshuka shimoni.30“Wakuu wote wa kaskazini na Wasidoni wote wako huko, wameshuka chini pamoja na waliouawa kwa aibu ijapokuwa kuna vitisho vilivyosababishwa na nguvu zao. Wamelala bila kutahiriwa pamoja na wale waliouawa kwa upanga na kuchukua aibu yao pamoja na wale wanaoshuka shimoni.31“Farao, yeye pamoja na jeshi lake lote, atakapowaona atafarijiwa kwa ajili ya makundi yake yote, wale waliouawa kwa upanga, asema Bwana Mungu Mwenyezi.32Ingawa nilimfanya Farao aeneze vitisho vyake katika nchi ya walio hai, Farao pamoja na makundi yake yote watalazwa miongoni mwa wasiotahiriwa, pamoja na wale waliouawa kwa upanga, asema Bwana Mungu Mwenyezi.”